PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Je unaweza kucheza Ngwasuma kuliko Queen Suzy?


KUTOKANA NA SABABU ZISIZOELEWEKA KUNA WATU HAWAJAWAHI KULEWA HATA SIKU MOJA. SASA NINGEPENDA KUWATAARIFU DALILI AMBAZO HUWA ZINAMJULISHA MTU KUWA KALEWA:
1. Kupoteza pochi na kushindwa kabisa kukumbuka iko wapi.

2. Kucheza nyimbo za Ngwasuma kwa kutikisa mabega huku umenyanyua mikono juu, na kujiona unacheza kuliko Queen Suzy

3. Kuwa na imani kuwa unaweza kumdunda mtu yoyote katika baa, tena hata wateja wote wakija kwa pamoja unaweza kuwafanyizia kitu mbaya, pia kuwataarifu kwa sauti kubwa kuhusu uwezo wako huo.

4. Kuweko bado baa alfajiri masaa matatu kabla ya muda wako wa kuingia kazini, na kuwa na imani kuwa pombe itakuwa imekutoka utakaporipoti kwa ofisi saa moja na nusu

5. Macho hayataki kukaa wazi.Lakini ni wazi watu wanavutiwa na sura yako

6. Kujikuta ghafla umekuwa bingwa wa kuvuta sigara

7. Ugomvi na kaunta kuwa kachakachua kinywaji mbona hakileweshi

8. Kila sentensi unaanza na maneno, ‘Naomba usinielewe vibaya….’

9. Kama hujafunga zipu, haikusumbui sana

10.Unavua viatu baada ya kugundua vinakufanya ushindwe kutembea
11. Kudai chenji mara mbili

Comments