HATUPIMI BANDO

8 August 2012

Je namba yako ya simu ina maana gani?


Utafiti umeonyesha namba yako ya simu ina uhusiano na tabia yako. Asilimia kubwa ya wenye namba zinazoishia;
0-wakorofi hawachelewi kuanzisha vagi, namba hii hupatikana sana mikoa ya kaskazini mwa nchi hii
1- wana huruma ukiwaomba credit wanakupa, mapedeshe wengi namba zao huishia na namba hii,
2- wanapenda kuimbaimba, wanakwaya wengi wamo humu
3- wanaakili sana ngoja nicheki namba yangu, nadhani niko kundi hili
4- waaminifu sana, huaga kwa nyumba ndogo kuwa wanarudi home na kweli wanaenda moja kwa moja home
5- wanapenda kuchekesha watu, kuna uwezekano mkubwa Masanja namba yake iko kundi hili, hata yule mama muendeshaji ya vikao mjengoni nadhani nae yumo humu
6- wasafi sana, hata viatu wanapiga kiwi mpaka soli, kitaalamu inaitwa,'NUMERO DU SHAROBAROQ'
7- wana sura za kuvutia sana, hebu cheki namba yako kama humo humu usijaribu kushiriki uMiss
8- hawanaga longolongo, namba hii nadra kupatikana katika anga za wanasiasa
9- wana aibu, hii namba imekutwa wanayo wacheza shoo wengi sana hapa nchini

No comments: