HATUPIMI BANDO

15 August 2012

Je mzazi unajua kusoma ripoti ya mwanano?


Ukiwa mzazi ni vizuri kuelewa namna ya kusoma ripoti za shule za mwanao. Hapa ni tafsiri halisi za nini walimu huwa wanamaananisha katika ripoti ya mwanao
1. Mwanao ana upeo wa hali ya juu wa kupata taarifa toka kwa wanafunzi wenzie (Mwanao kisha kamatwa mara nyingi akipiga chabo kazi za wenzie)
2. Mwanao na mchangamfu mwenye afya nyingi. (Mwanao hatulii mahala pamoja ni msumbufu)
3. Mwanao anaubongo wenye uwezo wa kutunga vitu vingi vipya (Mwanao muongo sana)
4. Mwanao anaonyesha tabia za utulivu usiotaka wala kutegemea usumbufu (Mwanao mvivu kupindukia)
5. Mwanao anaonyesha kipaji kikubwa cha kuwa mwanasiasa(Mwanao mbishi kupindukia)
6. Mwanao anakipaji cha kupenda kuzuru sehemu mbalimbali nje ya maeneo ya shule (Mwanao mtoro shuleni)
7. Mwanao ameweza kuendelea kuhifadhi tabia nyingi za wakati alipokuwa na umri mdogo. (Mwanao kikojozi)

No comments: