HATUPIMI BANDO

3 August 2012

Hata mimi nilikuwa nakutania tu

Mbaba: Hellooo
Swity: Heloooo mambo mpenzi
Mbaba: Pouwa uwapi nilikuwa nataka nikuone baadae
Swity: Dah niko mbali, nimekuja huku Mbagala kuna rafiki yangu kafiwa na mume wa rafiki yake wa dadake. Sasa tuko huko tutakesha.
Mbaba: Loh bahati mbaya, nilikuwa nataka tukutane nikupe lunch halafu nina ka Galaxy kapya nilitaka kukupa.
Swity: Poa basi ngoja nijipange nije, nikukute wapi?
Mbaba: Niko maeneo ya posta hapa, sasa utaondokaje huko na msiba je?
Swity: Kwani kuna msiba? Nilikuwa nakutania tu.
Mbaba: Hata mimi nilikuwa nakutania tu bye

No comments: