HATUPIMI BANDO

12 August 2012

Fundi gari limegoma

Mabiku kanunua gari jipyaa, otomatik, siku hiyo mchana kutwa akaliendesha vizuri sana. Ilipofika usiku gari likagoma kwenda. Siku ya pili mchana gari likazunguka vyema ilipoingia usiku likagoma kabisa kutembea, akaona amuite fundi. Baada ya kupata maelezo fundi akachanganyikiwa kabisa;
FUNDI: Yaani mzee sielewi, gari liwe linatembea mchana halafu usiku halitembei sijawahi kusikia tatizo kama hilo. Kwani huwa unaendeshaje?
MABIKU: Unajua hili gari wazungu wamelitengeneza liwe linaenda otomatik, sasa hapa kwenye gia ikiwa mchana unaweka kwenye D maana yake DAY hapo linaenda vizuri,  ikiwa usiku unaweka kwenye N maana yake NIGHT kusudi litembee usiku, sasa usiku halitaki kabisa au labda masaa ya Ulaya na huku yako tofauti?
FUNDI: Teh teh teh teh hahahahahahaha uwiiii mzee umenimaliza ngoja, ni kweli naenda leta spea, ntalazimika kumuagiza ndugu yangu yuko Sauzi aniletee, ni kama shilingi laki tano tu, kwa muda huu ifunge asichezee wala kuigusa mtu mpaka ntakapoishughulikia
MABIKU: Hakuna tabu fundi

No comments: