PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Daktari kazimia


Familia moja ilikuwa na bibi yao mzee sana aliyekuwa na matatizo ya moyo, hivyo wakawa na makubaliano na daktari mmoja awe anampitia na kumcheki hali mara kwa mara. Bibi akamwamini sana daktari. Siku moja Bibi akawatuma wajukuu zake wakamnunulie tiketi ya bahati nasibu, tiketi ikashinda zawadi ya kwanza ya shilingi milioni mia moja. Ndugu wakafanya kikao, wakawa na wasiwasi Bibi akipata habari za pesa hizo anaweza akashtuka akafa, hivyo wakaona wamwombe ushauri daktari, ambaye baada ya kusikiliza akawaambia wamwachie yeye atajua namna ya kumwambia Bibi bila kumshtua. Daktari akamwendea Bibi.
Daktari: Shikamoo Bibi
Bibi: Marahaba dokta wangu, mbona leo umekuja bila ghafla?
Dokta : Hahahahaha Bibi nataka nikuulize swali moja, kwa mfano umecheza bahati nasibu ukashinda shilingi milioni mia moja utafanya nini?
Bibi: Hahahaha, kwanza nitakata nusu nikupe wewe maana unanisaidiaga sana....DAKTARI AKAANGUKA AKAZIMIA

Comments