PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Breaking News...hatimae wanasayansi wa Bongo wavumbua kitu

Ndugu waandishi wa habari, kwa kweli nashukuru mkutano wetu muhimu hatimae umekwisha maana ulikuwa mgumu lakini wenye kuhitaji majibu. Wanasayansi wa Bongo tumekaa na kukuna vichwa vyetu kwa miaka mingi ili kupata kitu ambacho nchi inaweza kujivunia kuwa wanasayansi wake wamegundua, kitu kitakachoweza kuanzisha kupatikana akina Pythagoras wa Kibongo, akina Newton wakibongo, akina Einstein wa Kibongo, kitu ambacho kitatoa jibu ambalo litasaidia wanasayansi wengine duniani kuendeleza tulipofikia, na kweli pamoja na ubishi mkubwa wa kisomi uliofanyika. Ndugu waandishi wa Habari sasa kwa furaha kubwa tunaweza sasa kusema bila shaka yoyote kuwa wanasayansi wa Bongo tumegundua kuwa  BINADAMU NDIE MNYAMA PEKEE ANAEWEZA KUPATA KIGUGUMIZI

Comments