HATUPIMI BANDO

27 August 2012

BREAKING NEWS--KITIME KUWASHTAKI WALIOMTUHUMU UZEE KWENYE SAFEBOOK, I MEAN FACEBOOK

KITIME AKIWAZA SANA

Kwanza nichukue nafasi kusema asante ya hali ya juu kwa wote walionitumia salamu za heri kwa siku yangu ya kuzaliwa kwenye ukuta wangu wa FACEBOOK, hasa wale walioandika HBD, ambayo nimeambiwa ni kifupi cha Handsome Boy of Dar es Salaam umeona eee, ni wazi hawa wana akili sana wanastahili kupewa ukurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, ntaongea na Waziri husika, tukikutana kwenye duka la kofia umeona eee. Halafu sijui niongee kingleza, maana asilimia 96 ya mesej nilizopata leo ni za kingleza. Zote zimeanza na Happy Birthday, unaona ee, which means asilimia 96 ya marafiki zangu ni wazungu si unaona ee. And then naona ni wazungu kutoka nchi mbalimbali, si unajua kwetu Warusi , Wagiriki, Wataliano , Wamarikani, Waingereza na kazalika wote ni wazungu, umeona ee. Sasa nimegundua kuwa nina marafiki wazungu kutoka aina mbali mbali za wazungu kutokana na jinsi walivyomalizia ile Happy Birthday, wengine wamesema Happy Birthday Uncle, wengine, Ankle, Ankali, Ankar, Anko, Ango, Ankal umeona eee. Hawa asilimia 4 ambao ni waswahili wamenishangaza sana, bila sababu za msingi wameniita, Babu, Mzee, Mkongwe, Veteran, why? Nawapa siku saba waniombe radhi aua nawapeleka mahakamani na kuwadai shilingi billion 300 kama fidia umeona eeee, tusiharibiane CV hivihivi live. Kuna wale ambao bado naongea na mwanasheria wangu ili kuona hatua za kuwachukulia eti wamenitumia picha za keki, this is not for laugh, because if forexambo I am try to eat facebook, will you be happy? Ehh sema will you be happy? Zeafo tukutane tarehe kama hii next yia of koz ntakuwa nimelipwa fidia kutoka kwa hawa waharibifu wa CV kwa hiyo we will pariiiiiiiiiiiiii mpaka deibrek auvipi??? Si umeona eee...

No comments: