HATUPIMI BANDO

18 August 2012

Baa hii imekwisha niboa


Jamaa alikuwa bar anakunywa bia, alipotaka kuondoka kaunta akamdai malipo. Jamaa akamhakikishia kaunta kuwa amekwishamlipa, ikalazimika kaunta akubali. Jamaa akatoka nje akamhadithia rafiki yake kuwa kaunta msahaulifu hakumbuki kama kalipwa au la, rafiki yake nae akaingia akanywa na alipoanza kudaiwa nae akajitetea kuwa kisha lipa, huyu nae akatoka nje akakutana na rafiki yake wa zamani  Kingi, aliyekuwa nje anatengeneza pikipiki, basi nae akamhadithia na kumwambia kama anataka kunywa bia za bure aingie tu kwenye baa anywe halafu ajitetee kasha lipa. Kingi akaingia akaagiza akaanza kunywa, baada ya kuagiza bia ya tano, kaunta akamsogelea akaanza kumhadithia, ‘Unajua rafiki yangu leo siku ya ajabu kuna watu wawili wamekuja wamekunywa halafu wamejidai wamelipa wakaondoka, kwa kweli akija mtu mwingine akijidai amelipa safari hii namtwanga mingumi’. Kingi akajua mchezo unataka kumbadilikia, akawahi akajibu,’ Bwana ee nimekuja kunywa sio kusikiliza matatizo ya biashara ya baa, umekwisha niudhi hebu nipe chenji yangu niondoke, baa hii imekwisha niboa’

No comments: