HATUPIMI BANDO

31 August 2012

HAYA MLETENI YULE DEMU WENU


Jamaa kaingia bar kakuta kibao kaunta
;;;BIA BURE MWAKA MZIMA KWA ATAKAYEWEZA SHINDANO LETU;;;;;; akamuuliza kaunta kuhusu lile tangazo akaambiwa masharti yenyewe ni kuwa kwanza anywe dumu zima la gongo bila uso wake kuonyesha makunyanzi, kisha aingie chumba chenye mamba ambae anaumwa jino na kuling'oa halafu apande gorofani kuna chumba yuko mwanamke mmoja mkorofi sana amshughulikie.
JAMAA: Duh gongo dumu zima si uchizi huo.
Basi akaendelea kunywa bia zake zilipomkolea akamwambia kaunta hebu leta lile dumu la gongo. Akalinywa bila kukunja uso japo machozi yalikuwa yanamlenga. Alipomaliza akafunguliwa chumba chenye mamba akaingia, kukasikika kelele vurugu hatimaee kimya kikatawala, ile watu wanataka kwenda kufungua mlango wakijua jamaa atakuwa kaliwa na mamba, jamaa akatoka na michubuko ya hapa na pale lakini akiwa salama. Jamaa huku akiyumba kwa ulevi wa dumu la gongo,akamuuliza kaunta
JAMAA: Haya nishamshughulikia mamba wenu,sasa mleteni yule demu wenu mlisema anaumwa jino nimng'oe sasa hivi.

DOKTA WAKO FEKI

MUSA: Dokta wako feki
DOMI: kwanini?
MUSA: Si unakumbuka alikuwa anamtibu mzee Jailo ugonjwa wa figo, mzee wa watu akaja kuugua maini na akafa
DOMI: Sasa feki kivipi?
MUSA: Mi dokta wangu ukienda unaumwa kifua, basi ujue  utakufa kwa ugonjwa wa kifua. Ukienda unaumwa tumbo, basi kama kufa utakufa kwa kuumwa tumbo

JAMAA KALALA WAPI?

Mmama mmoja mbeya aliyekuwa hachoki kufuatia yasiyomhusu na kuyatangaza, alimuanzishia maneno jamaa mmoja mgeni kabisa mtaani. Baada ya kukuta gari ya jamaa nje ya baa moja, basi akaanza kueneza maneno;
MMAMA: Jamani huyu mgeni  mlevi sana, tena anaonekana analala baa maana gari yake utaikuta iko nje ya baa usiku kucha.... Jamaa aliposikia hizo tuhuma hakujibu kitu, lakini akaenda kulaza gari nje ya nyumba ya yule mama. Akawaachia wananchi waamue wenyewe huwa analala wapi

NATAKA KWENDA KUSOMA FINLAND


Watoto wawili wamerudi kwao na majibu ya mtihani wa mwisho wa muhula;
BABA: Safi sana naona umepata A kwenye masomo yote.
DIANA: Nataka kwenda kusoma AUSTRALIA
BABA: Na wewe Tina naona umepata F masomo yote, ndio nini hiki?
TINA: Nataka kwenda kusoma FINLAND

WEWE NI KICHWA MAJI

Asilimia 75 ya ubongo wa binadamu ni maji, pia asilimia 95 ya matango ni maji, huo ndio ukweli wenyewe. Hivyo basi kuitwa kichwa maji si tusi hata kidogo ni ukweli halali wa kisayansi. Sielewi kwanini watu wakiambiwa ukweli huwa wanaanza kukunja ngumi.

JE,WEWE NI MWANAUME WA KWELI?

LEO CHEKANAKITIME ILIKUWEKO UZINDUZI WA DUME CONDOM TUENDELEE KUCHEKA
Je, nani katesti? Halafu kama imetestiwa ndo kusema navaa iliyotestiwa? teh teh teh umeelewa eeee

Samahani u ziliisha ndo tukageuza n ikawa u. Siumeonaeeeee

Hili liboksi lina zile za wenye xxxxxxxxxxxxxxxxxxxlarge siunawajuaeeee

Umeonaeee

Teh teh teh itanikosti


MITIHANI YA KISIKU HIZI

MITIHANI YA KISIKU HIZI
 Jibu maswali mawili tu kati ya haya;
SWALI 1.-Lugha
Kabila la Wahehe huongea lugha gani?
(a) Kihehe
(b) Kirumi
(c) Kigagagigikoko
(d) Kisambaa
 SWALI 2-Sayansi
Chombo gani huonyesha picha za video?
(a) Pasi
(b) TV
(c) Radio
(d) Baiskeli
SWALI 3 -Jiografia
Jiji la Tanga liko katika nchi gani?
(a) Australia
(b) Canada
(c) Nigeria
(d) Tanzania

KWA WANAWAKE


UNATAKA NDOA YA HARAKA


MWISHO WA USHAROBARO

MWANZO WA MAJUKUMU, MWISHO WA USHAROBARO

NENDA NJE KAVUE

MKE: Hebu nenda nje kafue nguo
MUME: Jamani nje mvua inanyesha
MKE: Si uchukue mwamvuli

30 August 2012

ULISHAVULIWA TULIA

MKE: Kabla hujanioa ulikuwa ukinipa zawadi mbalimbali siku hizi sioni hata kanga
MUME: Uliwahi kusikia mvuvi anaendelea kumpa samaki chambo baada ya kumvua?

FOR CENSER COUNTING PEOPLE


29 August 2012

NTAKUNUNULIA DUNIA

MLEVI 1: Mi naweza kukununulia dunia
MLEVI 2: Huwezi
MLEVI 1; Kwanini nisiweze?
MLEVI 2: Sababu siwezi kukuuzia

AKILI NA PESA UTACHAGUA NINI?

TICHA: Kati ya pesa na akili wewe ungechagua nini? Haya Juma tuambie
JUMA: Ningechagua pesa mwalimu
TICHA: Mimi ningechagua akili. Sasa Juma kwanini umechagua pesa badala ya akili?
JUMA: Kila mtu huwa anachagua kitu ambacho hana

LINI UTAANZA KAZI?

MUME: Nashukuru Mungu kazini wamenipandisha cheo sasa ntakuwa na ofisi yangu mwenyewe, na wameniambia niajiri sekretari wangu mwenyewe.
MKE: Yote heri , ila kipengele cha sekretari nashauri uajiri mwanamke mnene mnene, mbaya mbaya, asiyejijali ili usije ukapata vishwawishi ukaharibu kazi.
MUME: Poa, unadhani unaweza kuanza kazi lini?

MWAMBIE UNAMDAI MILIONI

Jamaa alikuwa anamdai mwenzie laki tano lakini kukawa na kukwepana kwenye kulipa , akaona aende kwa mwanasheria;
JAMAA: Jirani yangu namdai laki tano inaonekana anataka kukwepa kulipa nifanyeje?
MWANASHERIA: Una ushahidi?
JAMAA: Kwa kweli sina tulipeana kindugu
MWANASHERIA: Basi muandike barua mdai shilingi milioni moja yako
JAMAA: lakini namdai laki tano
MWANASHERIA: Haswa, tunachotaka arekibishe hilo kimaandishi ili tuwe na ushahidi toka kwake mwenyewe

YOU HAVE FAILDED IN ENGLISH

BOYFRIEND: Hallooo
GIRLFRIEND: Hallooo
BOYFRIENDI: hearded you faileded English
GIRLFRIEND:Haa jamaa waongo sana  who tolded you?
BOYFRIEND:Your friendship Halima
GIRLFRIEND:She is lie sana, she is very lie

ONJA UONE KAMA UNA SUKARI

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?....Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka majimaji yaliyomo kwenye kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama ninakisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

NIKO KWENYE PUB KARIBU NA HAPO

Mke kampigia simu mumewe;
MKE: Uko wapi mpaka saa hizi hujarudi?
MUME: Unakumbuka lile duka la sonara, tulipita siku ile ukaona ile cheni nzuri sana?
MKE: Limefanya nini?
MUME: Unakumbuka siku ile nilikuwa sina hela ya kununulia ile cheni?
MKE: Ndio mume wangu mpenzi, nakumbuka
MUME:Basi niko kwenye kipub kilichokaribu ya hapo

BABU ANAKAIMBISHA KABINTI

BABU: Mtoto nakupenda sana, ukinikubali utafurahi
KABINTI: Akuuu, we mzee una miaka hamsini mi nina 19 wapi na wapi?
BABU: Nani ana miaka hamsini? Mimi nina umri wa miaka 25 na uzoefu wa miaka 25, kwa hiyo tumepishana kidogo tu.

28 August 2012

FLAT SCREEN TV

Madaktari wa hospitali ya machizi waliwapa wagonjwa mabox na kuwaambia watengeneze TV. Baada ya nusu saa kila mgonjwa akaambiwa alete TV yake, wote kasoro mmoja wakaja na mabox yao wakidai ni TV, huyu mmoja akaingia na karatasi tu, madaktari wakaona huyu kidogo akili yake imetengemaa. Wakamuuliza vipi mbona hukutengeneza TV? Akajibu,'Si hii hapa, akaonyesha karatasi, ila yangu Flat screen'

ONYO ONYO UKIANZISHA NGUMI SIKU HIZI SHAURI ZAKO,HAWAAMULII WANAWAHI PICHA ZA KUWEKA KWENYE FACEBOOK

ONYO ONYO ONYO

SIKU HIZI UKIANZA KUPIGANA USITEGEMEE WATU WATAAMULIA, SHAURI ZAKO. UKIANZA NGUMI WATU WANAWAHI KUPIGA PICHA WAWEKE KWENYE FACEBOOK NA BLOGS, SIKU HIZI HAKUNA KUAMULIA, UKILIANZISHA UTAJIJU UMEONAEEEEE

WAHI MUUJIZA TUMA VOCHA

Kuna kitu cha ajabu ambacho kwa kweli hata mimi sikielewi, ila tu naweza kusema miujiza inatokea. Binti mmoja alikosea akanitumia vocha ya shilingi 500, usiku ule kaka yake aliyoko Jahannesburg amemtumia shilingi alfu hamsini. Msanii mmoja maarufu amenitumia vocha ya shilingi alfu mbili, nusu saa baadae amepata pedeshee ambaye licha ya kutangaza kumuoa tayari amemkabidhi BMW mpya. Rafiki yangu wa huko Iringa amenitumia vocha ya shilingi alfu tano, biashara yake ya ulanzi imekuwa ghafla katika mwezi mmoja tu amekuwa wakala wa bia. Ni jambo la ajabu lakini liko wazi kuwa muujiza unakufuatia mara tu ukinitumia vocha. Nimeona niweke wazi hili jambo ili watu wengi zaidi muweze kutumia nafasi hii kupata muujiza wenu. Haya haya haya wahini kunitumia vocha maana huwezi kujua lini bahati hii itakata. 

JIRANI YANGU MJAPANI ANATWANGANA NA MKEWE


Majirani zangu Wajapan nyumba ya pili wako katika ugomvi mkali, ngoja niwaleteeni 'live'
MUME: Sukitaki  
MKE: Kowanini!
MUME: Toka a anji rodi roumi yakoo, (kipigo)
MKE: Mimi nakoundinda tinkouji! 
MUME: Na miaou kina tim kouji
MKE: chingogi
MUME: Yu ishna yukan nayi (.....jamaa analia) 
Yaani umeacha shughuli zako muhimu unaamini hii stori? Nimetunga tu hamna Kijapani wala nini hapa

BIG SOOOO, UNAFANYAJE PALE AMBAPO..........


UNAFANYAJE PALE  AMBAPO-
- Unapogundua jamaa uliyemtukana kwenye foleni ndiye mwenyekiti wa kamati inayokuinterview kwa ajili ya kupata kazi?
- Mbu anapotua kwenye kipara cha baba yako na wewe umewahi kutaka kumuuwa kwa kibao safi kwenye kipara hicho? Na kisha ukamkosa mbu huyo?
- Unapokuwa kwenye daladala na badala ya kutupa vocha uliyokwangua umetupa noti yako ya alfu na ndio ilikuwa hela yako ya mwisho?
- Umeme umekatika ghafla na wewe unawatukana wafanyakazi wote wa shirika la umeme bonge la tusi, tatizo ni kuwa baba yako anaefanya huko kaingia ndani ghafla na amekusikia?
- Dereva wa bodaboda uliyopanda anaanza kujibu mesej iliyoingia kwenye simu yake?
- Umeenda kuiba kwenye nyumba moja, mwenye nyumba kakushtukia na  katoka na panga anaanza kukufukuza, unaanza kukimbia unagundua kumbe ni nyumba ya Usain Bolt?
- Ulitaka kumpa ombaomba shilingi mia tano, ukiwa umeshampa unagundua umempa alfu tano?