PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Weeeeee staki tena kidogo nikamatwe na bosi


Jamaa wawili walikuwa wameajiriwa kwa Bosi mmoja, baada ya muda wakagundua kuwa Bosi wao alikuwa na tabia ya kuondoka saa 7 mchana na harudi tena mpaka kesho yake. Siku moja wakakubaliana nao wafunge kazi mapema waende zao nyumbani. Moja wao alifika kwake akapata muda mzuri wa kupumzika akaona raha akaazimia kuwa kesho yake lazima atoroke tena. Huyu mwingine kufika kwake kasikia sauti za ajabu toka chumbani kwake, alipochungulia ndani akamkuta bosi wake na mkewe, akafunga mlango haraka na kukimbilia kazini. Kesho yake mwenzie akamwambia tutoroke tena, jamaa akagoma akasema,' Weeee sitaki tena huu mchezo, jana kidogo nikamatwe na Bosi'

Comments

Anonymous said…
hahahahaaa babu jinga kweli huyo jamaa lol
Anonymous said…
daha jamaa alipataje kazi