HATUPIMI BANDO

18 July 2012

We nipe tenda mkuu


Jamaa watatu walienda kuomba tenda ya kujenga uzio wa nyumba ya serikali,
MJENZI 1: Mimi naweza kujenga uzio kwa shilingi milioni 2, vifaa milioni,wajenzi laki tano na mimi nitapata faida laki tano.
MJENZI 2: Mimi nanaweza kujenga uzio huo kwa shilingi milioni tatu, vifaa milioni, wajenzi milioni na mimi mwenyewe ntapata faida ya milioni. 
Mjenzi wa tatu akamwita pembeni mtoa tenda,
MJENZI 3: Sikiliza mkuu mi nataka milioni 12, milioni tano zako, tano zangu halafu tunamkodisha yule fala wa kwanza ajenge uzio, imekaaje hiyo?  Akapata tenda mara moja.

No comments: