HATUPIMI BANDO

22 July 2012

WARAKA WA KWANZA KWA MAKULUTA


Haya Jeshi la Kuienga Taifa (JKT), ndio hilo linakuja tena. Kwa kweli ni mahala ambapo wengine watapafurahia wengine watakesha wanalia, lakini mwisho kila mmoja atatoka na kitu kipya na kumbukumbu ya pekee  katika maisha. Lakini JKT ina masharti mengi, kwa hiyo nimeona nianze kutoa  WARAKA WA KWANZA KWA MAKULUTA’ ambao utaweza kuwasaidia ‘ makuluta’ watarajiwa kupata ahueni wakienda huko. Jambo la kwanza kuanzia siku utaingia katika eneo la kambi wewe utaitwa KURUTA, hili ni neno lililotokana na neno la Kiingereza ‘recruit’, usipaniki ukadhani linatoka kuleee pande anazotoka Lady nanihii wa Machozi. Ukifika utapewa namba na utajulikana kwa namba yako. Kila utakapofungua mdomo wako lazima umalize na neno AFANDE. Ukiulizwa unatoka wapi? Utajibu Dar es Salaam AFANDE, ukiulizwa uko Coy gani? utajibu,Coy A AFANDE, kimsingi utalitaja hilo neno mara nyingi mpaka hata usingizini utakuwa unaliota, usishangae ukitoka huko, hata demu wako akikuuliza ,’Bado unanipenda?” utajikuta unajibu, Ndio AFANDE. Lakini ni muhimu kuwa na akili na kujichunga sana ukiulizwa jina lako hasa kama jina lako ni Rungula, Mboya, Kichacha na majina kama hayo ambao ukiunganisha lile neno la AFANDE maana inaweza kuwa nyingine kabisa na ukaishia kupata adhabu kwa kusema kitu cha ukweli, kwa mfano ukiwa unaitwa Kichacha, ukaulizwa, Jina lako nani? Ukijibu Kichacha afande, unaweza ukaishia mahabusu, hivyo basi ni vema kukarabati majina ili yasilete utata. Katika waraka wangu wa pili italazimika niwaeleze msamiati wa JKT ili muweze kufahamu maana ya maneno kama , Jongomeo, Maslahi, Disko na kadhalika
Wasalaam ni mimi Afande

No comments: