PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Wako wajinga kuliko wewe

MUDI: Mke wangu ananidharau sana
KIDOA: Kivipi?
MUDI: Anasema eti hakuna mwanaume mjinga kama mimi
KIDOA: Huyo mama hajaona wajinga nini? Ona, ngoja nimuite yule dereva wa kibajaji ndio ujue duniani kuna wajinga. Kidoa akamuita yule dereva wa kibajaji
KIDOA: Aise hebu chukua hizi shilingi elfu tano, nenda pale kwangu kaangalie kama nipo
KIBAJAJ: Ndio mzee.. Dereva akaondoka huyooo
KIDOA: Unaona Mudi sasa ndio ujue kuna watu wajinga bwana
MUDI: Kweli yule mjinga, ningekuwa mimi ningechukua hela halafu ningekupigia simu nikuulize kama upo

Comments