PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Vua vua umegeuza kandambili

Mtu na mkewe waliingia kibanda cha mganga wa kienyeji kutafuta dawa kwa ajili ya mbaba aliyekuwa hawezi kutimiza majukumu yake kama mume. 
MGANGA: Nina dawa nzuri sana ni kanda mbili ambazo zitamaliza tatizo lenu.
 MUME: Hiyo siamini, kanda mbili na tatizo langu wapi na wapi?........Mganga akatoa kanda mbili;
MGANGA: Vaa uone kazi ya mizimu, mama jitayarishe hapa lazima kieleweke,dawa hii ina nguvu sana... Jamaa ile kuvaa tu alipiga ukelele akamrukia mganga akaanza kumvua nguo mganga, mganga alijaribu kila njia kuponyoka ikawa ngumu, hatimae akaanza kupiga kelele;
MGANGA: Vua, vua, umegeuza kanda mbili mamaeee

Comments