HATUPIMI BANDO

11 July 2012

Unampigia kelele Mungu nyamaza

Watu walikuwa kwenye maombi kila mtu akiomba yake kwa Mungu, mdada mmoja akawa anapiga kelele, Mungu nipe laki moja nimalize matatizo. Pembeni kulikuwa na jamaa anamuomba Mungu ampe milioni 50, lakini kelele za mdada zikawa zinazidi kuwa kubwa, zinamkosesha raha;
JAMAA: Dada samahani kwani unatatizo gani?
MDADA: Namuomba Mungu anipe laki moja tu nimalize matatizo
JAMAA: Huoni kuwa unapiga kelele Mungu anashindwa kutusikia si wengine? Hebu chukua laki yako nyamaza muache Mungu atusikilize wenye matatizo makubwa

No comments: