PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Umitoka kulikuli nyumbani?


Jamaa na rafiki yake toka kuliiiii kwa watani zangu walikuja mjini, walipopita sehemu fulani wakakuta tangazo, suruali 1,500/-, shati 500/-, suti 3,000. Wakakubaliana kuwa wakichukua mzio huo na kurudi nao kwao wakiuza ni bonge ya dili. Mmoja akamwambia mwenzie sasa kwa kuwa wewe kiswahili chako kibovu watatushtukia kuwa tumetoka kuliiii, wacha niingie mimi. Basi jamaa akaingia kwa mbwembwe sana,
Jamaa: Nataka vitu kadhaa toka dukani kwako, suti 100, mashati 1000, suruali 1000. Nifungie nasafiri navyo
Mfanyabiashara: He mzee umetoka kule nanihii?
Jamaa: Haa umejuaji?
Mfanyabiashara: Hii dry-cleaner bwana hatuuzi nguo hapa, tunafua na kupiga pasi tu.

Comments