PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Umenifungiaaaa


Mdada mmoja mwenye shughuli za kisanii anayeendesha Pub yake maeneo ya Kinondoni, siku moja alifunga Pub yake kama saa nane ya usiku, kafika kwake akiwa hoi, ile usingizi unaanza kumpata simu yake ikalia, sauti ya kilevi ikasikika;
SAUTI: Hallo mchumba, Pub yako unafungua saa ngapi?...... kwa hasira akakata simu. Baada ya dakika chache ikalia tena
SAUTI: Hallo we dada, saa ngapi unafungua Pub yako husikii?. Mdada akakasirika;
MDADA: Sikiliza wewe acha kunisumbua na ujinga wako hata ningekuwa nimefungua nisingeruhusu mlevi kama wewe kuingia shenzi
SAUTI: Ngoja , mbona unapaniki, nani kakwambia nataka kuingia? Mi nataka kutoka umenifungia

Comments