PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Ni pombe hizo mke wangu

Mke alikuwa na mpenzi wake kitandani aliposikia funguo kwenye kitasa cha mlango wake, akamwambia mpenzi wake;
MKE: Usipaniki we lala kimya jamaa mlevi sidhani kama atakuona.  Mume baada ya kuingia akavua nguo nae akapanda kitandani, si akashangaa kuona akihesabu miguu iko sita.
MUME: Mbona naona miguu sita?
MKE: Hizo pombe zako zitakuua, mbona mi naona miguu minne tu, hebu amka halafu uhesabu tena. Jamaa akatoka kitandani na alipohesabu tena akakuta miguu minne
MUME: Samahani mke wangu, ni kweli kuna miguu minne tu. Haya tulale sori tena ni pombe tu mke wangu

Comments