HATUPIMI BANDO

19 July 2012

Naomba unisukume

Ilikuwa usiku wa manane, mtu na mkewe walikuwa wamelala usingizi ghafla wakasikia mtu anagonga mlango. Mume akaamka na kufungua mlango;
MUME: Vipi tena usiku huu?
MLEVI: Samahani mzee nina tatizo naomba ukanisukume. Mume akafunga mlango na kurudi kulala. Jamaa akaendelea kugonga.
MKE: Si umsaidie mwenzako, hata wewe unaweza ukapata tatizo usiku. Mume akaamka akavaa na kukubali kusindikizana na mlevi akamsaidie.
MUME: Mbona sioni gari?
MLEVI: Subiri, na hatimae wakafika mahala kuna mabembea, mlevi akapanda moja;
MLEVI: haya nisukume


No comments: