HATUPIMI BANDO

16 July 2012

Mwizi wa tishu????Toka kwa Anko Tom wa Tanzania Daima…………JUMATATU ya wiki iliyopita nilikwenda katika ofisi moja jijini Dar es Salaam ambayo mara kwa mara huwa nafika hapo kutokana na shughuli zangu za kila siku za kutafuta riziki.
Mara baada ya kufungua mlango wa ofisi hiyo nilikaribishwa na bonge la zogo hivyo nikajikuta nimeduwaa kwa muda wa dakika kadhaa nikiwa sina la kufanya zaidi ya kuwaangalia na kuwashangaa hao waliokuwa wakizozana.
Zogo hilo liliendelea hadi pale mwanadada mmoja aliyekuwa na muonekano wenye sifa zote za mtu mtanashati na mstaarabu alipoondoka ndipo hali ya hewa ya ofisi hiyo ilipotulia na mimi nikapata nafasi ya kuuliza ili nipate kujua sababu za kutokea kwa zogo hilo ambalo nina hakika kama isingekuwa ni sehemu ya ofisi za serikali, basi lazima sisi wapenda mchezo wa masumbwi tungepata burudani hiyo bila ya kulipa kiingilio chochote.
Nilipoelezwa sababu za ugomvi huo kuwa ni wizi wa tishu (karatasi za chooni) kwa hakika nilishindwa kuamini kama kweli huyo bibiye aliyetoka hapo ndiye mtuhumiwa mwenyewe au kasingiziwa!

No comments: