HATUPIMI BANDO

20 July 2012

Mume kasafiri wiki nzima


Bosi alikuwa anasafiri akamwita dereva wake Sam amsindikize airport. Wakiwa njiani kwenda airport, Bosi akakumbuka kuwa kasahau document muhimu nyumbani kwake akaamuru warudi kwake. Alipoingia chumbani kwake akakuta mkewe yuko bafuni anaoga, akanyata ili ‘am surprise’, akafungua mlango wa bafu taratibu na kumshika mkewe. Bibie akiwa na mapovu ya sabuni mwili mzima akaanza, ‘He Sam mara hii umeshamfikisha yule fala airport?, Usiwe unakimbia hivyo sweetie mie sipendi , halafu haraka ya nini tuko wenyewe wiki nzima’.

No comments: