PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Msinibabaishe, leteni mia tano yangu


Mjingamjinga mmoja alinunua tiketi ya bahati nasibu kwa shilingi 500 akashinda shilingi milioni 20. Haraka akaenda ofisi ya bahati nasibu, nao wakacheki na kukubali kuwa tiketi yake imeshinda.
Mjingamjinga: haya nipeni milioni 20 zangu.
Bahati nasibu: Sheria yetu hapa tunakupa leo milioni na kila mwezi unakuja kuchukua milioni moja mpaka ziishe.
Mjingamjinga: Msinibabaishe nipeni nilipeni milioni 20 zangu
Bahati nasibu: Bwana hiyo ndiyo sheria yetu
Mjinga mjinga: Bwana e kama ni hivyo basi chukueni kitiketi chenu nirudishieni mia tano yangu wajinga wakubwa.

Comments