HATUPIMI BANDO

23 July 2012

Mpenda Udaku Sugu


Kuna watu wanapenda udaku, utakuta mtu anaenda kilomita tatu akasikilize tu akina mama wakibishana ili awe na taarifa 'live'. Jamaa mmoja alikuwa anadai akamkuta mdaiwa wake barabarani, akamwambia leo tumekutana lazima unilipe, mdaiwa kamwambia jamaa hunipati najiua akachukua kisu akajichoma akafa. Mdai akasema sikubali nakufuata hukohuko, akajichoma kisu nae akafa. Mpenda Udaku sugu aliyekuwa anawaangalia pembeni akasema sikubali lazima nione mwisho wa hili picha 'live', nawafuata hukohuko, akaokota kisu naye akajichoma akafa

3 comments:

kabali faraji said...

hahahahahaha!hatariiiii

kabali faraji said...

hahahahaha!hatariiiii

Yasinta Ngonyani said...

Kaaaazi kwelikweli ...