PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Mke wangu kanambia nimwage pombe dah

Mke wangu alirudi home akanambia kaokoka kwa hiyo eti chupa zangu za konyagi zote nimwage. Kwa kuwa nampenda nilimkubali nikatoa nje chupa zote, nikafungua chupa ya kwanza nikaimwaga yote kasoro glasi moja nikainywa, nikachukua chupa ya pili nikaimwaga yote kasoro glasi moja ambayo niliinywa, nikachukua chupa ya tatu nikaimwaga glasi chupa nikainywa, nikachuka glasi ya nne nikaimwaga yote nikainywa, nikachukua konyagi ya tano, nikainywa glasi yote nikaiweka chupa kwenye konyagi nikainywa. Nikachukua glasi nikainywa na chupa ya konyagi. Aaaa go away

Comments