HATUPIMI BANDO

6 July 2012

Mi nilizikwa jana tu...

Polisi katika doria wakamkurupusha mwizi wakafukuzana nae akaingia makaburini, kufika huko akavua nguo akakaa juu ya kaburi, polisi wakaja;
POLISI: Aise umemuona mtu kapita hapa anakimbia ni mwizi tunamsaka
JAMAA: Aise mi mgeni nimezikwa jana tu, hivi nipo hapa juu ya kaburi langu napunga upepo ndani huko joto sana, labda muwaulize hayo makaburi hapo mbele....polisi hawakusubiri amalize walikuwa wote wameingia mitini

No comments: