PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Mbona Mungu kaninyima?


Siku ya kufunga shule mzazi mmoja kaenda na mwanae shule, sherehe zikaanza wanafunzi wakawa wanapewa vyeti na zawadi kadri ya ubora wa mambo yao, mtoto wa jamaa yetu hakutajwa hata jina. Mzazi akawaangalia wale watoto waliofanya vizuri akamwambia mwanae;

Baba: Wale ndio watoto, mbona Mungu kaninyima? Wakaondoka na kuelekea kituo cha basi kuwahi basi la kwenda kwao. Wakati huo huo wazazi kadhaa wenye magari wakawa wamekuja kuwachukua watoto wao, mtoto akawaangalia wale wazazi nae akasema;

Mtoto: Dah wale ndio wazazi mbona Mungu kaninyima

Comments