PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Masikini Wema


Ndugu Mhariri,
Nimeona niandike kwenye gazeti lako ili unisaidie katika tatizo langu, maana kwa kweli nimeona umesaidia wengi wenye matatizo kama yangu. Juzi nilikuwa naenda kazini nikamuacha mume wangu nyumbani anaangalia TV, gari langu likazima kama kiasi cha kiliomita moja toka nyumbani. Nikaona nitembee mpaka nyumbani kumwomba mume wangu aje anisaidie kutengeza gari. Kwa msahangao wangu nilipofika nyumbani nikamkuta mume wangu yuko na chumbani na msichana wa kazi wa nyumba ya jirani. Mume wangu ana miaka 43, mimi nina miaka 39 na msichana huyo ana miaka 19 hivi.Tumekuwa katika ndoa kwa miaka 10. Nilipomuuliza mume wangu alikubali kuwa uhusiano wao umekuwa ukiendelea kwa miezi sita sasa, nifanye nini mimi?.
Wema

Jibu
Dear Wema,
Nimesoma vizuri barua yako na naweza kukushauri ifuatavyo, kwa kusema ukweli gari kuzima ghafla linaweza likawa limesababishwa na mambo kadhaa, aidha betri haichaji, au petroli imekwisha au fyuzi imekatika Ni vizuri ukaanaza kuangalia kama filta ya petroli ni safi na jaribu pia kucheki plagi. Nategemea jibu hili litakusaidia
Mhariri

Comments