PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAUFUNGA MDOMOWANGU

NAUFUNGA MDOMOWANGU
NAUFUNGA MDOMO WANGU

Marehemu alipenda watu

Jambazi mmoja alikuwa kauwawa na polisi, siku ya mazishi yake majambazi wenzie wakajikusanya kwa siri ili kuhudhuria msiba. Wakafika wakakuta msemaji wa familia anatoa sifa za marehemu;
MSEMAJI: Marehemu alikuwa ni mtu wa watu alipenda watoto, alikuwa masaada mkubwa kwa wanafamilia na majirani zake. Ni wazi saa hizi yuko peponi akifurahi na malaika.
JAMBAZI 1:(akawaita wenzie) Nadhani tumekosea, huu si msiba wa jamaa yetu twendeni tukapeleleze msiba wake uko wapi

Comments