PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Mama ndoa imenishinda

Mdada baada ya kuolewa kwa siku chache kampigia simu mama yake;
MDADA: Mama mi ndoa imenishinda huyu mwanaume ananipigia kelele hata vitu vidogo
MAMA: kwani vipi tena?
MDADA: Jana nimemtengenezea soseji 2 badala ya kushukuru kaanza kulalamika eti natumia hela hovyo
MAMA: He mbona shida, bei ya soseji mbili tu kelele
MDADA: Sio bei ya soseji ni microwave
MAMA: Sasa sielewi
MDADA: Nilitaka kumpashia moto zile soseji kwenye mfuko wameandika tumia microwave, ndio nikakodi taxi nikaenda supamaketi nikanunua microwave mpya , mume wangu apate soseji za moto ananipigia kelele.

Comments