HATUPIMI BANDO

20 July 2012

Kuzaa bila maumivu

Mama mmoja mja mzito alikwenda kwa mganga wa kienyeji ampe dawa ya kuondoa maumivu wakati anazaa. Mganga akampa punje tatu za karanga akamwambia akisikia maumivu atafune karanga moja maumivu yatahamia kwa baba wa mtoto. Mumewe akakubali kubeba mzigo wa maumivu. Siku ya kujifungua mama alipoona maumivu yanaanza akatafuna punje moja, maumivu yakapotea, mumewe akamwambia,'Nyie wanawake kumbe huwa mnajidekeza tu, mbona sioni maumivu yoyote'. Baada ya muda maumivu yakamrudia yule mama akala punje nyingine, matokeo yakawa vilevile, mume hakusikia chochote akawa anacheka sana tu. Hatimae akaanza kupata maumivu makali ya kujifungua akatafuna punje ya mwisho na kujifungua salama bila maumivu kwake wala kwa mumewe. Wakarudi nyumbani na furaha, furaha yao ikakatishwa kwa kukuta kuna msiba wa kijana wao wa kazi aliyekutwa amefariki. Majirani walidai alikuwa analalamika kwa maumivu makali kama vile anataka kuzaa.....

No comments: