PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Kumbe unasoma shule

Mwanangu,
Nategemea umzima. Kuna kitu lazima niseme. Kila mara ulikuwa ukirudi likizo unatuambia uko chuoni, tena ulikuwa mkali sana wakati tulikuwa tukisema unasoma shule, ulitusahihisha kuwa wewe ni mwanachuo. Nakumbuka kuwa uliwahi hata kupigana pale kilabuni na mtoto wa Gaspa alipokuita mwanafunzi. Juzi nilikuja unaposoma sikukuta, ila wenzio wakanielekeza unaposoma, kwa kweli nimekasirika sana kumbe we bado ni mtoto wa shule, wamenionyesha mpaka shule unayosoma. Nasema hivi rudisha hela zote nilizokupa ulizokuwa unasema unalipia chuoni. Sitaki maneno yeyote mengine
Mimi  baba yako
Mnyalu

Comments