PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Baba Ubaya anamjua kila mtu

Baba Ubaya alikuwa anajisifu sana kuwa yeye anajuana na watu wote muhimu nchini na hata nchi za nje, bosi wake akamtaka aache uwongo naye akasisitiza kuwa anamjua kila mtu. Siku hiyo bosi wake akamuuliza unamjua Mbunge Sugu? Ubaya akajibu, 'Sana tu', Bosi akaamua kumpeleka mpaka Dodoma, kufika kule Mheshimiwa kumwona tu akasema, 'A h Baba Ubaya uko huku? Karibu mbona hukunambia kuwa unakuja?'. Bosi akashangaa lakini akajua hilo lilikuwa bahati. Baba Ubaya akasisitiza ,'Bosi we taja tu mtu mi namfahamu naye ananifahamu' Bosi akamuuliza, 'Unamfahamu Waziri Mwakyembe?', Devi akamwambia Bosi wake waende Bungeni, kufika tu Mheshimiwa kumwona Baba Ubaya akamwambia,'Vipi wewe Ubaya, niko bize kidogo ila ntakutafuta'. Bosi sasa akajua Baba Ubaya ni mkali. Hatimae akaamuuliza kama Baba Ubaya anamfahamu Waziri Mkuu, wakaamua kumtafuta wakamkuta akihutubia mkutano, Baba Ubaya akajipitisha hatimae akapanda kwenye jukwaa, Bosi akaona Baba Ubaya anasalimiana kwa furaha na Waziri Mkuu, kilichommaliza Bosi ni pale alipomsikia Muhindi aliyekuwa karibu nae akimwambia Mhindi mwenzie, 'Hane ona ile Baba Baya ile rafiki ya Rais ya India, pale juu iko salimiana na nani?"

Comments