HATUPIMI BANDO

31 July 2012

Konda kaharibu kitandani

Konda alikuwa kakasirika sana, abiria alikuwa kagoma kulipa nauli akisisitiza eti yeye ni denti, wakati kila mtu alimuona ni mtu mzima, konda akamkunja jamaa, wakapigana sana, abiria alipoona anapigwa akaanza kukimbia, konda akamfukuza abiria akaaingia kwenye shimo, konda alipofika pale akakuta yeye hawezi kuingia kwenye shimo, kwa kisirani akaamua amkojolee humohumo kwenye shimo, wananchi waliokuwa karibu wakamhamasisha konda, 'Mnyee huyo, konda mnyee', konda akavua suruali na kulenga lile shimo na kuachia kitu. Hapo ndipo sauti ya hasira ya  mkewe ikamuita, ikiambatana na makofi, konda akazinduka toka usingizini, akakuta kishaharibu mambo yote kitandani

Its cold and refreshing, I mean the beer


30 July 2012

Haneee Juma ve leta vageni nataka

Juma kaenda kuomba kazi ya uboi kwa muhindi, mambo hayakuwa mabaya kwa wiki mbili za kwanza. Siku hiyo ndugu zake bosi wakamtembelea bosi, Juma akaambiwa apange meza ya chakula, akaweka vizuri sahani, visu, vijiko lakini akasahau kuweka  uma. Wageni wote wakawa wamekaa kwenye viti vyao , Juma akiwa nje anapumzika, ghafla akasikia;
BOSI: Hanee Juma lete nyuma..... Juma hakuamini alichosikia,
JUMA: Umesemaje Bosi?
BOSI: Ve apana sikia, lete nyuma vageni nataka...
Bosi hakujua na mpaka leo hajui ni kwanini Juma alimtandika kama vichwa sita vya mfululizo

Waume 5,000/-, wanawake bureee

Haya matangazo kwenye kumbi za disko yana utata enzi hizi;
 DISCO DISCO DISCO  
WANAWAKE BUREEEE
WANAUME 5,000/-
 Swali wale jamaa zake Cameroon wako kundi gani?

Tanga Kunaniii??????????


Happy Birthday cheka na kitime.blogspot

Toka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano Vodacom Bi Joseline Kamuhanda, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, na mwendeshaji wa blog hii John Kitimeakipokea cheti cha tuzo la Vodacom.
Leo Blog hii imetimiza mwezi mmoja, tena kwa kuwa na heshima kubwa ya kuwa imeweza kuchekesha watembeleaji zaidi ya 30,000. Tuongezeke kucheka ndio raha iliyobaki kabla mafisadi hawajaingia kunyanganya hata hicho, pia siku ya leo blog ya historia ya muziki wa dansi inayoendeshwa na John Kitime imekuwa moja ya blog kumi ambazo zimepata Tuzo la Vodacom la umahiri katika dijitali. Karibuni www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com

Simba Kabakwa


Nyani alikuwa anapita karibu na kisima cha maji akamkuta simba kainama anakunywa maji. Nyani kwa uhuni wake akamnyatia simba akambaka, alipomaliza akamsukumia kisimani akakimbia, alijua simba akitoka huko kuna kimbembe kitatokea, katika kimbia yake akamkuta mzee mmoja kavaa kofia kakaa kwenye kigoda anasoma gazeti maarufu la udaku. Akamtisha mzee wa watu, mzee akakimbia akadondosha gazeti na kofia, nyani akaivaa kofia akakaa kwenye kigoda nae akaanza kujifanya anasoma gazeti. Simba akatokea kachukia kweli, akamuona mtu kavaa kofia anasoma gazeti la udaku;
Simba: Oyaa umemuona nyani mmoja kapita hapa?
Nyani: Yupi? Huyo aliyembaka simba kisimani?
Simba: Ayaaa usinambie imeshaandikwa kwenye magazeti ya udaku?

29 July 2012

Waif aliingia ghafla........

Jamaa kaenda hospitali kutibiwa, kavimba  jicho;
DOKTA: Vipi ulifanya nini hapa?
JAMAA:Ahh bwana mambo yetu yale, nilimkumbatia hauzgelo,
DOKTA: Hapo sijaelewa kumkumbatia hausgelo inaletaje kuvimba jicho
JAMAA: Si waif akaingia ghafla, we nitibu bwana acha maswali.

Mnanitekenya mwenzenu

Jamaa walikuwa wanaosha maiti kuitayarisha kwa mazishi, ghafla maiti ikaanza kucheka;
MAITI: Kwi kwi kwi kwi Mnanitekenya mwanzenu jamani ahh...............Mlango ulikuwa mdogo

Swaga za kutoa sadaka jumapili-


Bosi anatisha bwana


Kila shetani na mbuyu wake, jamaa anamuogopa bosi huyooo dah

Mke akikukosea humpigi

Jamaa alikuwa akimpiga mkewe mapema asubuhi Jumapili ya leo hapo mtaa wa pili. Katika watu waliokuwa wamezungunguka kujaribu kuzuia timbwili lile akatokea mshauri mmoja;
MSHAURI: Mheshimiwa mke akikukosea humpigi
MKE: Mume wangu msikilize mwanaume mwenzio
MSHAURI: Mheshimiwa mke akikukosea humpigi, ila unamuolea mke mwenzie
MKE: Mume wangu usimsikilize huyo we nipige tu

USAFI NI MUHIMU

Kutokana na maradhi mengi yanayotokana na uchafu tunashauri matumizi ya toilet paper hii ambayo kwa kweli inasugua vizuri sana. Tumia hii kwa afya yako

Hivi Amina tuko wapi?


Jamaa kaamka nyumbani kwake asubuhi baada ya kuwa alirudi kalewa sana jana yake,kichwa kikiwa kinamgonga kabla akili haijaamka sawasawa;
Jamaa: Amina, tuko wapi hapa?
Mkong'oto wa nguvu ukamshukia, tatizo lilikuwa dogo tu, jina la mkewe ni Rehema.

Teh teh Porn area.... lugha ya wenyewe ohooooo


Tafadhali maji haya si ya kunywa


28 July 2012

Ndege ilipokwama hewani

Waswahili wawili walipanda ndege yenye injini 4. katika kati ya safari nahodha akawataarifu kuwa injini moja imezima kwa hiyo watachelewa kufika kwa robo saa. Baada ya muda nahodha akatangaza tena kuwa injini ya pili imezima kwa khiyo watavhelewa nusu saa.
MSWAHILI  1: Zikizima zote itakuje?
MSWAHILI 2" Itakuwa mbaya maana italazimika tukwame hukuhuku juu mpaka mafundi waje
MSWAHILI 1: Dah hiyo itakuwa soo tutachelewa mambo mengi sana

Kaanzie hospitali ya vichaa

Jamaa kawahi alfajiri kwenye ofisi ya chama cha siasa, akawa mtu wa kwanza kuonana na vigogo ofisi zilipofunguliwa;
JAMAA: Wakubwa najua chama chetu ni cha Kidemokrasia, hivyo basi nataka kujiunga ili uchaguzi ujao nigombee urais, sasa naomba ushauri nianzie wapi?
 KIGOGO: Kaanze kwa kujiandikisha hospitali ya vichaa

Maliza Bia wambie wakupe bili


Jamaa yangu Devi hana raha, mchana leo alipigiwa simu na Bosi wake ambae alikuwa safari, yeye mwenyewe wakati huo alikuwa bar akipata moja moto moja baridi saa za kazi;
Bosi: Vipi Devi? Mnaendeleaje na kazi hapo ofisini?
Devi: Mkuu hapa mambo safi sana tuko bizi sana, watu leo wamekuwa wengi utafikiri wametumwa bosi, hakuna hata nafasi ya kupumua
Bosi: Ok, Unaweza kunisaidia kitu kimoja?
Devi: Hakuna tabu  Mzee sema tu.
Bosi: Haya maliza hiyo bia yako, halafu nenda kaunta niulizie bili yangu changanya na bili yako

27 July 2012

Nawaza kelele za CHADEMA mwanangu

Kigogo alipojiona sasa yuko juu, akaamua kumfwata kijijini kwao mama yake, akaenda na helikopta akamchukua akampeleka mjini, walipofika huko akampeleka kwenye hoteli ya kifahari wakala vizuri, kisha kwa kutumia Vogue lake akampeleka mama yake kuona bungalow lake jipya, wakati wote huo mama yake alikuwa kimya hasemi kitu. Kigogo akamuuliza mamayake;
KIGOGO: Mama mbona kimya husemi lolote hunisifii mi mwanao kwa yote haya?
MAMA: Mwenzio nawaza kelele za CHADEMA Bunge likianza

Kumbe una nyumba ndogo

Baada ya uchaguzi wa serikali za mtaa mgombea karudi kwake amenuna.
MKE; Vipi matokeo?
MUME: Nimeangushwa vibaya
MKE: Umepata kura ngapi?
MUME: Kura mbili
MKE: Mshenzi mkubwa kumbe una nyumba ndogo hapa mtaani leo utamtaja

Nikishinda bahati nasibu itakuwaje?

Jamama karudi home na furaha kubwa;
MUME: Aise nambie kama nikishinda bahati nasibu utafanyaje?
MKE: Ntataka unigawie nusu halafu, ntadai talaka nisepe
MUME: Basi una bahati leo, nimeshinda shilingi alfu kumi, nusu yako hii na talaka yako hii sepa salama.

Sweety unaona lile BMW


Pedeshe yupo Coco Beach na wale wa kwenye luninga.
Pedeshe: Mtoto ulisema birthday yako next week?
Hani: Yeah
Pedeshe: Nataka nikununulie kitu unikumbuke daima, unaona lile BMW jekundu pale?
Hani: Wauuuu ukinunulia lile mbona watazima sigara zao, yu are soooo sweet, unajua kumhendo msichana, love kiss kiss,
Pedeshe: Subiriiii, unaona lile BMW jekundu, basi nimekununulia rangi ya kucha inamech rangi na lile BMW