PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Unataka niwe wa 20?


Mdada mmoja mke wa mtu alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja aliyekuwa akimtaka kila siku, hatimae akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe, we mkubali tu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu.
Mdada akafuata masharti ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na yule bwana , mumewe akiwa tayari na panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona ana makovu makubwa kifuani na mgongoni;
MKE: He mbona una makovu hivyo
JAMAA: Niwe mkweli mie nina tatizo sana la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nimeshafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania nimewaua.
MKE: He jamani….jamaa akaendelea kuvua nguo alipomaliza mdada akaanza kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni, mume kabana kimya, kila jitihada za mdada kupunga mkono hazikupata majibu mpaka jamaa kamaliza shughuli zake akatokomea.
MKE: Jamani sasa ndio nini? Mbona hukutoka
MUME: We we we, mwenyewe umesikia kasha ua 19 unataka niwe wa ishirini?

Comments

Majoy said…
Hahahahaaaa hiyo kiboko!