PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Unamjua Hasani Makolokocho wewe?


Jamaa alianza kujisifu sana kazini kwake;
Jemsi: Wiki ijayo nafanya mtihani, ni miezi sita sasa nafanya masomo ya jioni, nimejua mengi sana, we unamjua Speke?
Devi: Hapana simjui
Jemsi: Huyo ndie mzungu wa kwanza kuuona mlima Kilimanjaro, ungekuwa unasoma masomo ya jioni ungemjua huyu.
Jemsi akawa kero kazini kwa maswali yake.
Jemsi: We unamjua Graham Bell?
Devi: Hapana simjui
Jemsi: Huyo ndie alikuwa mtu wa kwanza kutengeneza simu, ungekuwa unaenda kuchukua masomo ya jioni ungemjua.
Siku moja Devi akamwita Jemsi;
Devi: Jemsi unamjua Hasani Makolokocho?
Jemsi: Huyo ndie anaetembea na mkeo kwa miezi sita sasa, ungekuwa huendi kuchukua masomo ya jioni ungemjua

Comments