PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Toka Magazetini


Mwananchi newspaper by Hamida Shariff, Morogoro
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harison Mwakyembe amefanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu Manispaa ya Morogoro na kufanya ukaguzi wa mabasi ya abiria ambapo  mabasi matatu aliyaamrisha yalipe faini ya Sh250,000 kila moja kutokana na makosa mbalimbali likiwamo la kutokuwa na dereva wa akiba………Pole Mkuu unahitaji pia kuwa na Waziri wa akiba mabasi karibu yote haya dreva wa akiba, kwa kuwa wanansubiri waziri ndo aje awacheki Kwani tandiboi sio dreva wa akiba? ila matandiboi wa siku hizi masharobaro mno, wenzao zamani walikuwaga lazima wawe wachafu na mabingwa wa kushuka gari liko kwenye mwendo na kudandia likiwa kwenye mwendo na ilikuwa lazima basi liwe na kigogo chini ya kiti, cha kusaidia breki Tanzania Daima by Na Irene Mark 
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, anamwomba Mungu amuoteshe ndoto za kuwa Rais wa Tanzania…………Ehhh Mungu nioteshe ndoto na mimi za kuwa na mihela mpaka benki za Uswisi ziwe zina niogopa


Tanzania Daima By Ashura Jumapili
 MWALIMU Alfred Sitayo ( 32 ), Msubi mkazi wa Kibeta amehamishia maabara ya shule ya sekondari Nyakato iliyoko Manispaa ya Bukoba katika kituo chake cha kutoa masomo ya ziada (tuition).
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Philp Kalangi, amesema Alfred Sitayo alikamatwa Juni 18 mwaka huu akiwa na vifaa vya maabara, vitabu mbalimbali, kemikali za maabara ya kemia na viti ambavyo ni mali ya Shule ya Sekondari Nyakato……..teh teh teh   wengine huhamishia madawa kwenye famasi zao, wengine huhamishia kodi za wananchi  kwenye akaunti zao za Uswisi, wengine huhamishia mapenzi kwenye nyumba zao ndogo kila mtu anakula kivyake

Comments