PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

Lipstiki kwenye vioo


Shule ya sekondari ya wadada fulani hapa mjini ilikuwa na tatizo la wadada kubusu vioo vya msalani na midomo iliyojaa lipstick, jambo ambalo liliudhi uongozi wa shule kwa kuwa vioo vilijaa mirangi kila siku.Wanafunzi waliitwa kwenye mkutano wa shule na mfagizi akapewa ruksa kuongea.
MFAGIZI: Jamani kila siku mnabusu vioo kule chooni na kuacha lipstick kwenye vioo, naomba niwaombe mpunguze maana kwa kawaida huwa natumia maji ya chooni kuosha vile vioo sasa maji ya chooni yameaanza kuwa tabu kupata..........Kesho yake hakuna aliyebusu kioo.

Comments