HATUPIMI BANDO

27 June 2012

Nimewazika woote

Kundi la wanasiasa lilikuwa linafanya ziara vijijini bahati mbaya basi lao likapinduka. Mzee mmoja mkulima alipofika pale na kuona tu hali ilivyokuwa , akaanza kuchimba kaburi kubwa na kuwazika wale wanasiasa wote. Siku mbili baadae polisi wakafika kuchunguza ule mkasa mzima, na mzee aliyefanya maziko alikuweko;
POLISI: Mzee wewe ndiye uliyewazika wanasiasa hawa?
MZEE:Ndio ni mimi
POLISI: Kwa hiyo hata mmoja hakuwa hai?
MZEE: Kuna wachache walianza kujitetea kuwa wako hai, lakini si unajua uongo wa wanasiasa tena, sikuwaamini nikawazika wote.

No comments: