HATUPIMI BANDO

28 June 2012

Kizunguzungu


BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Arusha kwenye mkutano fanya mipango yote
SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Arusha kwenye mkutano
MUME (anampigia nyumba ndogo): Mambo safi, wife anaenda kikazi Arusha jitayarishe tujirushe
SMALL HOUSE (anamwambia mwanafunzi wake wa twisheni): wiki hii nina kazi fulani hakuna twishen mpaka wiki ijayo
MWANAFUNZI (anampigia simu babu yake (BOSI)): Babu hakuna twisheni wiki hii nakuja kwako
BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Arusha mjukuu wangu atanitembelea
SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Arusha
MUME: Aise mpenzi jamaa haendi mipango imeharibika
SMALL HOUSE (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida
MWANAFUNZI: Babu twisheni iko, nakuja wiki ijayo
BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Arusha iko palepale

No comments: