HATUPIMI BANDO

27 June 2012

Chura kiziwi


Msomi mmoja alikuwa anafanya utafiti, akamchukua chura akamwambia 'Ruka', chura akaruka mita 4, msomi akaandika katika kitabu chake kuwa chura mwenye miguu minne huruka mita 4. Kisha akamkata mguu mmoja na kumwambia 'Ruka' chura akaruka mita 3, msomi akaandika kuwa chura mwenye miguu mitatu huruka mita 3. Akamkata mguu mwingine na kumwambia aruke , chura akaruka mita 2, akaandika kuwa chura mwenye miguu miwili huruka mita 2, kisha akamakata mguu mmoja, na chura akaruka mita moja, msomi akaandika chura mwenye mguu mmoja huruka mita moja. Hatimae akamkata mguu wa mwisho, na kila alipomwambia 'Ruka' chura hakuruka, msomi akaandika kuwa katika utafiti wake amegundua chura akikatwa miguu yote huwa anakuwa kiziwi.

No comments: