HATUPIMI BANDO

30 June 2012

Kila nikiota kitu kinakuwa kwee...kinakuwa kweli

Kari yangu
Jamaa yetu alikuwa mahakamani kashtakiwa kwa kosa la mauaji. Akaruhusiwa kuanza kujitetea;
MANGI LUI: Mheshimwa mi ninatatiso kubwa, kila nikiota ndoto inakuwa kwee.. inakuwa kweli. Niliota mke wangu kasaa mapacha kweli akasaa mapaa...mapacha. Nikaota duka langu wamefunja, kweli wesi wakaja wakafuu..wakafunja. Mwesi uliopita sinikaota kari yangu mpya imeungua, siku mbili badae si ikaungua. Sasa nimelasimika kumuua huyu jamaa si usiku niliota ananibaka, inkekuwa wewe ungekubali?

Muulize hata baba

MAMA MWENYE NYUMBA:Jamani chupi zangu sizioni zinaenda wapi? We dada au umechukua wewe?
MDADA WA KAZI: Akuu mi sivaagi muulize hata baba

Kuna mamba hapo nimewafuga


Jamaa kenda kwenye bwawa la maji lililokuwa nyuma ya nyumba yake akateke maji, kufika huko kakuta kuna  akina mama kadhaa wanaogelea kwenye bwawa;
JAMAA: Nyie tokeni humo kwenye bwawa langu
AKINAMAMA: Hatutoki mpaka uondoke
JAMAA: Poa, isiwe tabu naondoka. Mi nilikuwa nawaletea chakula mamba wangu ambao nimewafuga humo……..

Haiwezi kuwaka hii

Maprofesa kadhaa wa chuo cha ufundi walikaribishwa katika uzinduzi wa ndege mpya, wakakaribishwa kwenye viti vya ndege wakafunga na mikanda. Walipopewa maelezo kuwa ndege hiyo ni matokeo ya project ya wanafunzi wao wenyewe, maprofesa wote walitimka nje kabla ndege hata haijawashwa, kasoro mmoja tu akabaki kwenye kiti;
MWANDISHI: Mzee wenzio wote wamekimbia mara baada ya kuelezwa kuwa ndege hii imeundwa na wanafunzi wenu, sasa wewe haukukimbia kwanini Mzee?
PROFESA: Sikuona sababu ya kukimbia kwa kuwa kama imeundwa na wanafunzi wetu sidhani hata kama inaweza kuwaka

Redds Miss Kanda ya Kati iliyofanyika MajajiDodoma nilikuweko 'live'

Majaji walitoa uamuzi ulikubaliwa na wote hongera

Mmoja wa washiriki akiwa katika vazi la ubunifu alilotuambia lilibuniwa na mama yake mzazi, hongera mama mzazi kwa kivazi

Twanga Pepeta walikuweko na hatimae kunipa lifti ya kurudi Dar. Hongera Twangaz na Kupepetaz hasa.................teh teh

Washindi wa Redds Miss Kanda ya Kati 2012...Hongereni pia hongera kwa Kiinglish chenu

Mdomo kama tairi la trekta

Mke alikwenda kulalamika kwa mumewe kuwa kuna jamaa mgeni jirani kamtukana kuwa ana mdomo kama tairi la trekta. Mume akapandisha na kuapa kutoa adhabu kali sana atakapokutana na huyo mshenzi. Siku walipokutana mume kanywea maana jamaa alikuwa baunsa wa ukweli;
MUME: Mambo jirani?
JIRANI: Mbona poa sana tu
MUME: Jirani nasikia ulimtukana mke wangu kuwa ana mdomo kama tairi la trekta
JIRANI: Ndio
MUME: Ahahha, tairi la mbele au la nyuma?
JIRANI: La nyuma
MUME: Ahaa nilidhani ulisema la mbele, inaonekana mimi na wewe tunawaza sawa, ila tu sijamwambia wife, si unajua akina mama wanavyoweza kupanik.

Nina baba wengi

Siku moja kabla ya mtihani wa insha mwalimu aliwataarifu wanafunzi wajitayarishe kwani kwenye mtihani atataka waandike insha kuhusu mtu wao wa karibu. Devi akajitayarisha usiku kucha kuandika kuhusu rafiki yake. Walipoingia kwenye mtihani mwalimu akawaambie watunge insha kuhusu Baba. Devi akachanganyikiwa....insha yake hii hapa chini.....
Mimi na baba wengi sana. Wengine wavulana wengine wasichana. Huwa napenda kucheza na baba zangu wote. Lakini ninaempenda zaidi anaishi mtaa wa pili toka kwetu. Kuwa na baba wengi huleta furaha kwani hata siku moja huwi mpweke...MWALIMU KAZIMIA

Kuna mtu kanionea kofia yangu?

Mgonjwa mmoja alitoka kwenye operesheni  alipopata fahamu akajikuta yuko kwenye chumba kina wagonjwa wengine wawili,
MGONJWA 1: Dah nashukuru Mungu operesheni yangu imefanikiwa
MGONJWA 2: Usiwahi kushukuru hawa jamaa waliwahi kusahau sindano tumboni kwangu
MGONJWA 3: mie walisahau pamba ikalazimika nirudie tena operesheni.....ghafla yule daktari aliyefanya operesheni akaingia mle chumbani
DOKTA: Vipi mnaendeleaje? Kuna mtu kanionea kofia yangu jamani?........MGONJWA 1 akazimia palepae

Demu wangu paka

PANYA 1: Nshawahi kunywa sumu ya panya na hakikutokea kitu
PANYA 2: Mi huwa nacheza kiduku kwenye mtego na haufyatuki
PANYA 3: Demu wangu paka, na ana mimba yangu

My baby anataka BMW new model

Hiki sasa kimbembe, nahitaji ushauri wa ziada. Binti kanijia juu, wenzake wote wana 'babies' aina za BMW, Lexus, yeye anacho hiki kigari ambacho ni aibu hata kutoka nacho, hata wenzie wakiongelea magari ye anakimbilia chooni, pia wenzie wana nyumba za kodi si chini ya milioni kwa mwezi, ye anadhalilika na nyumba ya laki tano kwa mwezi. She wants to change na kwenda na wakati. Yaani anashindwa hata kupiga simu mbele ya wenzie with that old model Blackberry, si watamcheka? Imagine watu wa magazeti ya udaku wakigundua TV ya chumbani kwake ni hizi 'cheap' za 1.5m, si itakuwa skendo?
Me, I am wondering sijui nilipue bomu gani? Wabunge wenyewe wamekuwa noooma wanafuatalia hata vimilioni vitano sita, yaani tunabanana mno, kuna kajiloan nakaservice ndio kananiletea shida kidogo, any one with 60m ntalipa hata kwa interest. Please advice.

29 June 2012

Naomba adhabu ya kifungo tu

Jamaa alikuwa na kesi nzito ya mauaji, ikafikia wakati wa kutoa hukumu akahisi wazee wa baraza watamuona ana hatiana anaweza akanyongwa, basi akampata mzee mmoja wa baraza akamhonga ili ashawishi wenzie wasimpate na kosa la mauaji ya kukusudia maana atanyongwa, ila japo liwe kosa la mauaji bila kukusudia ili afungwe tu. Kweli baada ya siku tatu wazee wa baraza wakakubaliana kuwa jamaa aliua bila kukusudia, Jaji akampa adhabu ya kifungo cha  miaka saba, akashukuru. Alipopata nafasi ya kuongea na mzee aliyemhonga;
MFUNGWA: Mzee nashukuru sana nategemea sikukupa kazi nzito
MZEE: Loh ilikuwa kazi nzito sana, wenzangu wote walikuwa wameona huna hatia hivyo kuwabembeleza wakubali kuwa umeua bila kukusudia ilikuwa ngumu sana.

Kalibuni


Mimba hii ya nani?

"Utanambia leo mimba hii ni ya nani, mi nagharamia miezi yote hii kumbe mimba si yangu"

Kumbe umesema Uyaya

Binti alirudi kijijini baada ya miaka 5.
BABA: We mwanaharamu umeondoka hapa kwa miaka mitano hukutaka kutuandikia barua wala kutuma salamu unajua ulimtesa sana mama yako?
BINTI: Baba niliona niwe kimya nilikuwa nafanya kazi ya umalaya
BABA: Ayaaaaaa umetia aibu kubwa familia yangu lohh, ntatembelea wapi mimi?
BINTI: Sawa baba, lakini nimemletea mama sanduku la nguo na kanga 20 na pesa, na hii hapa ni hati ya kiwanja nimemnunulia. Na wewe baba nimekununulia hilo gari nililokuja nalo na nimekufungulia akaunti, ina pesa utaweza kulima vizuri na kujenga nyumba nyingine ya kisasa.
BABA: Ulisema ulikuwa unafanya kazi gani?
BINTI: Umalaya
BABA: Unajua nilisikia vibaya nilidhani umesema Uyaya, pole na kazi mwanangu

Tamko la Jumuiya ya Madikteta


Jumuiya ya Madikteta tumeamua kutoka hadharani kuwatetea wanyonge. Nyie wanyonge mnapata tabu sana kwa hiyo sisi tumeamua kuwatetea. Tuna mikakati kabambe ya kuhakikisha mnakombolewa kutoka hili dimbwi la njaa kali, uonevu, dhuluma, na kunyimwa haki zenu za kimsingi kwa ujumla. Ili kuweza kuwaletea raha ya milele tutafanya yafuatayo;
1. Tutazuia chakula kisipikwe popote (mnajua hili ni kiboko maana wanaowanyanyasa wakiona mna kufa kwa njaa watapanik, hivyo watapanga mikakati ili chakula kipikwe)
2. Tukiona kuna dalili za chakula kupikwa mahala fulani tutafanya chini juu mpango huo usifanikiwe ili muendelee kufa kwa njaa, msingi hapa ni ‘objective’ kufa mtu mmoja hapa na pale siyo main issue. Tunajua mtatuelewa na mtakuwa na sisi katika kipindi hiki kigumu cha kutafuta njia ya kuwapa raha ya milele, mpaka tone lenu la mwisho la damu.(hapa tuwapongeze wapishi wote waliogoma kupika, maana wakifa watu wengi ndo ushindi wetu utakaribia)
3.Jumuiya ya Madikteta tungependa kuwataarifu kuwa ‘off course’ na sisi tuna kitu tutapata katika kuwakomboa, maana hatimae tutakuwa na magari, mishahara mikubwa, nyumba za kisasa, likizo Ulaya, lakini hivi ni vitu vidogo sana kulinganisha na ambacho hatimae mtapata maana itakuwa raha ya milele, hakuna kufa wala nini mtaishi mpaka mchoke
4.Tuungeni mkono kwa kuonyesha kuwa mnateseka na kufa wengi kwa njaa kwenye vyombo vya habari, hii itasaidia sana watu kushika adabu na kutuachia tupate tunachotaka, yaani furaha na raha yenu ya milele bila kufa

 IMETOLEWA NA MPASHA HABARI WA
JUMUIYA YA MADIKTETA DUNIANI KWETU

Wamama natoa onyo, punguzeni ufisadi


Ufisadi unatajwa sana katika mali kama ardhi, na pesa. Utasikia watu wanalalamika ohh Mwenyekiti anahodhi eneo kubwa sana la ardhi peke yake wakati wengine hawana eneo, au ohh jamaa anahodhi akaunti kubwa ya vijisenti wakati wananchi wengine wakiwa hawana hata hela ya kula. Kuna ufisadi ambao uko wazi ila watu wanaukwepa kuupiga vita.
Sensa ya mara ya mwisho hapa nchini,  ilionyesha wazi kuna uhaba mkubwa wa wanaume hapa nchini, sasa unakuta wamama wanahodhi mwanaume na kukataa katakata kushirikiana katika matumizi  kwa ushirikiano na wamama wenzie, huu ni ufisadi wa hali ya juu. Acheni uchoyo, tumieni bidhaa hii adimu kwa ushirikiano, amani na upendo. Nawasilisha hoja


Toka Magazetini ndani ndani kabisa


Kizimbani kwa wizi….Nipashe

Na Mwandishi wetu

28th June 2012Mfanyabiashara, Ajastina Kabume (23), amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la wizi.

Mwendesha mashitaka mratibu wa Polisi, Denis Mujumba, alieleza mbele ya Hakimu, Karimu Mushi kuwa majira ya saa 12 maeneo ya Tabata Liwiti manispaa ya Ilala, mshitakiwa aliiba vitu vyenye thamani ya Sh. milioni 1,399400 mali ya Priscus Venanc.

Mshitakiwa amekana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana na kesi yake imeahilishwa hadi Julai 11, mwaka huu itakapotajwa tena……….Hapa wahusika walikuwa wamechoka maana kuna makosa kibao humu, kubwa ni  hii mali walioyoiba walibebaje? Labda na meli kadhaa………milioni 1,399400 duh mwanawaneToka Mtanzania
SUALA la uadilifu kwa watumishi wa umma, limendelea kushuka baada ya watumishi wa Serikali katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kujiuzia magari ya Serikali aina ya Land Rover 110 kwa Sh milioni 2, huku thamani ya gari hilo ikiwa ni zaidi ya Sh milioni 120.
Mbali na gari hilo ambalo linadaiwa kununuliwa na mmoja wa watumishi katika Wilaya ya Kibondo, gari jingine limenunuliwa na Mwanasheria wa Wilaya, D. Ruhamvya, aina ya Nissan Patrol lenye namba za usajili SM 2976 kwa Sh milioni 3…….Sisemi kitu mamana sijui hali ya gari ilikuwaje. Pengine wamenunua scrapper?Toka Tanzania Daima
MBUNGE wa Micheweni, Haji Khatib Kai (CUF), amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikilalamikiwa kwamba zinachochea vitendo vya zinaa kwenye vituo unavyopiga kambi…………Mhhhhhh haya tena, itakuwa lile joto la Mwenge

Toka Tanzania Daima
HOSPITALI ya Regency ya Dar es Salam imeanzisha programu kabambe ya upasuaji wa maradhi mbalimbali ya tumbo kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kutumia kamera……….Dah nawaza tu picha za utumbo wangu ziki 'wikiliki' kwenye magazeti ya makorokocho

28 June 2012

Kwanini walaliane?DOGO: mama naomba nikalale kwa akina Helena, mama yake amesema ataturuhusu tulale chumba kimoja mmoja juu mwingine chini
MAZA: Kasema nini? Mshenzi mkubwa huyo, hebu twende…. Maza akafunga kibwebwe tayari kwa valangati
MAZA: We mama Helena mbona huna akili kwanini unataka kuniharibia mtoto wangu mshenzi mkubwa wewe?
MAMA HELENA: Jamani kwani nini?
MAZA: We umesema watoto waje kwako wakalaliane ndio nini? Mwanamke huna haya weweeeeeeee
MAMA HELENA: Jamani  we mtoto mi nimekwambiaje
DOGO: Umesema nije nilale kwenu na Helena, moja juu mwingine chini.
MAMA HELENA: Jamani Mama Dogo, kuna kitanda cha ghorofa mtoto moja analala juu mwingine chini haaa mwanamke weweee.

Mi sio mwizi

Mwanamke mmoja alipita katika kichochoro kimoja chenye giza nene kule Tandale ghafla akatokea mtu na kisu;
JITU: Oyaa simama hapo hapo....yule mwanamke akasimama lakini akaanza kucheka kwa nguvu.
JITU: We mwendawazimu nini? unacheka nini?
MDADA: Nakucheka wewe, umenisimamisha mimi sina simu, sina hata senti tano, utaiba nini sasa?
JITU: Hahahahaha nani kakwambia mie mwizi?

Kamkonga kako kadoooooogo

Jamaa alikuwa anaoga porini ghafla akakuta amezungukwa na tembo waliokuwa wakimuangalia kwa makini;
JAMAA: Nyie vipi mnashangaa nini?
TEMBO: Dah Kamkonga kako kadoooogo, unapumuaje?

Mi sina bahati kama mke wangu

Walevi watatu walikutana baa;
Mlevi 1: Hii baa nzuri lakini sio kama ya mtaani kwetu. Pale kwetu kuna baa ya Kimaro ukinunua chupa mbili , Kimaro mwenyewe anakunulia moja nyingine
MLEVI 2: Mtaani kwetu kuna baa ya Gano, hapo ukinunua moja na Gano anakunulia ya pili
MLEVI 3: Mtaani kwetu ndio kiboko, kuna baa ya Mzee Komba ukifika akikuchagua, anakununulia bia mpaka ulewe kisha anakupeleka kwenye gesti yake anakupa mtu wa kulala nae
MLEVI 1: Hapo kiboko, we umeshawahi kuchaguliwa?
MLEVI 3: Bado mi sina bahati sana, lakini mke wangu kisha chaguliwa mara 2 wiki hii peke yake.

Kiserengeti boi


Mtu na mkewe walikuwa bado wamelala asubuhi, mtu akapiga hodi mke akaenda kufungua mlango, si akamkuta Serengeti Boy wake,
MKE: Unataka nini we mpumbavu?
MUME: Nani huyo unamtukana?
MKE: Kuna mtu hapa anakichwa kama nenda urudi badae
Serengeti boy:Nawewe pua kama poa
MUME: Nani huyo anamtukana mke wangu?
MKE:Miguu kama masaa mawili
Serengeti Boy:Masikio kama sichelewi
MKE: Ondoka hapa mjinga we. Akafunga mlango