HATUPIMI BANDO

16 January 2018

MHARIRI MLEVI WA CHEKA NA KITIME BLOG ACHAMBUA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO.....vibamia hoyeee, ndio habari ya mjini soma hapa

 Kwa wale ambao Kingleza not richabo, ni kuwa hawa jamaa ambao ndio waliotuletea mifuko ya plastiki sasa wenyewe wameanza kuipiga marufuku  kwenye maduka yao. Unajua huku kwetu plastiki ziko kila mahala, vikombe, sahani, mifuko, viatu, dahh hizi vitu zinaharibu mazingira kishenzi yaani, wajukuu zetu watapata tabusana


 Hahahahaha  sio ishu, wavulana mbona nao wanang'ara kwa kuvaa milegesheo? Chupi zao zinang'ara kila mahala. Tena wanajitahidi suruali zikitaka kupanda wanaziteremesha ili chupi zing'are. 

 Ok hii ni habari nzuri sana maana ukitembea mitaa mingi Dar es salaam utakuta marundo ya takataka hazijabebwa hivyo wananchi waige mfano na kuwasha moto hizi taka ili mji  uwe msa, uwe msafii.

 Jamani acheni uchonganishi , yaani hapa inaonekana jamaa kipato kimeongezeka, wenye nyumba watapandisha bei, wenye madeni watadaiwa,  vibinti vile vipenda noti vitaanza usumbufu, kwani si mngesema Vigogo waongezewa majukumu si ingekuwa poa? 

 Aise namshauri aende baharini akaoge saa tisa usiku. Babu yangu aliwahi kunambia kuwa mikosi ikikuandama kaoge baharini saa tisa ya usiku, tumia sabuni ya unga, ukitoka hapo uko freshhhhh

 Ukisema neno 'mengine' unamaananisha kuwa si yale ya awali, au umeongezea yale ya awali, sasa dahh, sijui niseme nisiseme? Inanikumbusha Trump anahangaika kujitetea kutokana na kusema hakusema waliyosema amesema


 Oyaa nyie Singida vipi tena? Kwanini unamshika simba pabaya? Ndio mchezo gani mnaanza siku hizi? Mi nilijua kuwa shughuli yeni ni moja tu kucheza soka, sasa hii kushikana pabaya imetokea wapi? Kumbukeni kuna serikali, muulizeni Gigi mane yaliyomkuta, mpaka akalia, eti zea iz no fridom.

 Ushauri wa bure..... kule Kawe kuna daktari wa meno aliwahi kuziba pengo langu mpaka leo niko fresh kabisa mwaka wa pili. So mkitaka kuziba hilo pengo mnibip ntawapigia kuwaelekeza kwa yule daktari mdada hivi

 Sasa tumefikia pabaya watu wanatafuna mpaka Halmashauri? Yaani mishikaki yote ile kule Butiama wanaiacha wanaanza kutafuna Halmashauri? Hii ndio Tanzania tuliyofikia? Naziomba mamlaka za madawa na chakula kutoa tamko, hawa watu wanaweza kudhurika sana, Hivi mamlaka ya chakula imetoa go ahead watu watafune halmashauri? 

 Unajua vibamia vimepata kiki sana  siku hizi, kila siku vinatajwa, vinatrend Insta, facebook, tweeter, whatsap, sasa vimeibukia kwenye tiba, kula vibamia unapona magonjwa kumi. This is gud nyuz,  Vibamia hoyeeeee

Ebwanaeee hao huwa hawa ahidiwi kitu, hawasahau hao, unajichimbia shimo ndugu yangu, au we mgeni mitaa hii, hao toka babu zao huwaga hawana simile, kauli mbiu yao DAIMA MBELE, usipoleta ubingwa utaniambia kitakachokukuta

15 January 2018

CHEKA NA KITIME YACHEKA NA VICHWA VYA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO.......msanii maarufu amkuna mwenzie

 Oyaa nyie wasanii acheni hizo, kwanini we Bushoke unamkuna Ray C? Sio vizuri kukunanan hadharani mnaona sasa mmetoka ukurasa wa mbele wa magazeti 'serious'. Yaani badala ya kutupa ishu za mbolea imesambazwa vipi mnawababatiza wanawaangalia mnavyokunana, ngoja nije hapo hapo tuonane laiv

14 January 2018

CHEKA NA KITIME YABISHANA NA MAGAZETI YA JUMAPILI 14 JANUARI 2018.....wapiga kura walikuwa wengi au wachache? Nani muongo? anadoo


 Vikija vichwa vya habari kama hivi mi huwa napiga anadoo, ndio nijue kipi kinasema ukweli
Ana ana ana do
Kachanika pasto
Isplingi matingo
Kajamba, ushuzi unanuka, tena sana, sana kabisa.

Mzee ohoo unajua siku hizi kusema ukweli itakukosti? Ohoo mi mwenzio nimenyamaza kimyaaa, hawachelewi matusi instagram hao. Waoga kweli wanaweka majina feki insta halafu wanaanza matusi. Unajua hata ngumi zao hazivutii

 Dabi ndio nini? Ngoja nicheki kwenye kamusi au ngoja nigugo

 Tafsiri sentensi hii kwa kiingleza, jibu andika inboksi

 Aise mngeenda Mikumi kabisa sababu kule kuna simba wengine wengi wanaishi poa tu hawana gundu wala nini. Labda wangewapa dawa, unajua gundu baya sana, yaani mtu unaweza kukosa magoli, samahani unaweza kukosa hela hivihivi

 Jamani hawa si wana hospitali za miujiza mbona hazifungwi? Kila siku wanawapa watu dawa za kimiujiza, si lazima hapo na fedha za kimiujiza ziwepo, mbona wanagawa mashamba ya kimiujiza, wanaahidi magari ya kimiujiza, kupasi kimiujiza, kuoa kimiujiza, kuzaa kimiujiza......................

 Haya mambo mengine nafunga mdomo maana yake maraisi wanakuwaga wakali sana ukisema hili neno la kung'oka, pale kwetu tuna Rais wa walevi mtaani, tulipomwambia muda umeisha amepatikana mkali zaidi ngumi zikawaka moto. Kuhusu hili sisemi neno

 Mzee mzee nimeshakwambia hawa jamaa wakianza kukujibu utakimbia. Huku kuwa legelege ni kutokana na mambo mengi, si unakumbuka enzi ya madansi ya Moro jazz au Kubano uliwahi kumuona mwanaume ana kata mauno? sasa siku hizi wanakata mauno hata mpirani unategemea nini, ili ukate miuno vizuri si lazima uwe legelege?. Ila mi nasema tu sijasema wachezaji legelege nawaogopa, wataenda nitukania instagram

 Welkam bak Babu watu tulikumiss, watu walikutungia nyimbo, stori, wengine wanajiita jina lako, kumbe ile ilikuwa utangulizi kubwa zaidi inakuja? Haya Babu. Watu shangilieni babu babu babu

 Inategemeana, ila ngoja nijue kisa kwanza, nisije kuwa nadandia treni kwa mbele

 Hahahahahaha hii kali kumbe na Manabii wana kuwa na Mahasimu wao? Mi nilidhani simba na yanga tu, au team Kiba na team Diamond. Sasa na manabii nao ? Vipi wafuasi wao wanapeana vijembe insta? Hahahahaha dah Jumapili nzuri sana hii

 Watakuwa wameumia maana sakafu kwenye mahakama zetu huwa zinakuwa imara sana, poleni wachungaji. Kwa hiyo Jumapili hii makanisa kadhaa tutakuta wachungaji wana bendeji puani? Ngoja nikazunguke 

 Aise hivi Yesu akirudi akute mnatumia jina lake kuwapanga watu foleni wanalipa ndio mnawaombea, si mtakula mikwaju nyie kama walivyokula mikwaju wale waliogeuza sinagogi nyumba ya kufanyia biashara? Halafu na waumini na nyie ni jipu, wapi iliandikwa kuwa kuombewa unalipa. Huyo anae kuombea anaomba, halafu we unamlipa ili aombe?

 Nipeni hizo hela mnazotumia kufanya utafiti niwape jibu, mahala kwenye shida lazima hii itokee, sorry I am speak in English. Give me ze money it is you for research, ze peoples is hungry therefo it is kill it self and it is kill ze azas.

Una uhakika? Mbona kuna galizeti linasema wamejaa mpaka pomoni. It iz because you are mzungu you are not see peoples , because peoples zey are afraiding of mzungu so zey ranaway

13 January 2018

CHEKA NA KITIME YABISHANA NA MAGAZETI 13 JANUARI 2018 ....kuna mtu atamlipa Mrema bilioni 20 sababu ya umbeya

 Yaap kuna watu wamemzulia eti kafa, lazima alipe mtu huu mkwanja, kuna mtu umbeya utamponza. Watu mmezoea sana mnaingia mitandaoni na kutangaza watu wamekufa wakati wenyewe hawajapanga hivyo. Mtakoma sasa, mtauza mali za ukoo wenu wote bilioni 20/- parefu kudadadadadadadadadeki

11 January 2018

HATA MIMI LEO NDIO MARA YA KWANZA KUMPASUA MTU

Dokta kaingia chumba cha mgonjwa anaesubiri kwenda kufanyiwa operesheni,
DOKTA: Vipi mbona unaonekana umepanik sana?
MGONJWA: Kwa kweli sina raha hii ndio operesheni yangu ya  kwanza, naogopa sana
DOKTA: Usiogope bwana, mi mwenyewe pasonalii ndio ntakae kufanyia hiyo operesheni.
MGONJWA: Loh nashukuru sana, Dokta umeshawahi kufanya operesheni kama hii?
DOKTA: Hapana leo ndio mara yangu ya kwanza kumpasua mtu, lakini usihofu, chuoni nilikuwa napasi sana mitihani

CHEKA NA KITIME YABISHANA NA MAGAZETI 11 JANUARI 2018 ....kuna watu watakaangwa wiki hii, tukae mkao wa kuwala na chipsDah sasa hawa wakiaangwa si itafaa kuwe na chips kavu pembeni, chachandu kwa wingi. Manake nyama ya kukaanga inafaa kusindikizwa na chachandu ndio inateremka. Ila najiuliza kwanini wasikaange kuku? Au wakaange mayai hivyo ndivyo tulivyozoea kula na chips

10 January 2018

TUTOTO TWA SIKU HIZI TUKOROFI SANA

Kila mtu anapenda watoto wachanga. Hata jitu ambalo huwa mara nyingi halicheki na mtu liko siriaz wakati wote likikutana na katoto kachanga utakuta linaanza kutabasamu, tena likikabeba katoto kachanga utaona nalo linageuka kuwa litoto. Utaona linaanza kuongea na katoto kachanga lugha za ajabu kabisa utadhani wanaelewana, utasikia, ‘Shum Babu toto shum babu, au shum bibi, shum antii aijigijigijigi, awawawawa, abububujijiji’ na maneno mengine yasiyoeleweka eti ndio mtoto atacheka. Leo niwape siri, mnajua kwanini vitoto huwa vinacheka sana? Vitoto vichanga vimezaliwa na akili sana, sasa huwa vinacheka kuona baba zima au mama zima halijui kuongea vizuri, kitoto kinajisemea moyoni, ‘Huyu mkubwa mzima badala ya kuongea mambo ya maana eti anasema abujibujibujibuji’ kimsingi watoto wachanga wanawacheka sana, muwe mnaongea nao kikawaida, sawa ndugu zangu?
Leo niwape ushauri wababa wenzangu kuhusu taratibu  mbalimbali za kufwata kabala ya kucheza na watoto wachanga, kama nilivyosema vitoto vichanga vina akili sana,  hivyo basi sio kuanza kuvibeba kabla ya kujitayarisha. Najua wabishi wameshakaa mkao wa kubisha, lazima saa hizi wanasema kimoyomoyo,’ Hakuna kitu kama hicho, watoto ni malaika’. Mi nasema sawa hebu nisikilizeni kwanza. Wababa wenzangu, sharti la kwanza usicheze na mtoto mchanga ambaye ndio kwanza katoka kunyonya wakati umevaa shati la au koti lako la bei mbaya, hakikisha imeshapita japo nusu saa tangu amenyonya ndipo uanze kumrusharusha. Watoto hawa wajanja sana, wakijua kuwa umevaa kitu cha bei mbaya  watakutaim na kutumia nafasi hiyo kukucheulia maziwa na kama hukujiangalia vizuri unaweza ukaingia kwenye daladala na michirizi  ya maziwa ya mgando mgongoni.
Sharti la pili linahusu wale ambao hupenda kucheza na watoto kwa kuwanyanyua juu ya vichwa yao, kabla hujaanza kamchezo hako, hakikisha mtoto kavaa nepi. Katoto kakijua una kamchezo hako, katajifanya kanacheka sana na kufurahi kila ukikanyanyua juu, kumbe huo mtego, iko siku ukikanyanyua juu kama hakana nepi katakutaimu na kukukuharishia kichwani, chunga sana, maana inawezekana wakati huo mdomo wako uko wazi. Hutu tutoto twa siku hizi tunaanzaga ukorofi tumboni.


9 January 2018

CHEKA NA KITIME YABISHANA NA MAGAZETI 9 JANUARI 2018....eti Simba sio riziki acheni hizo bwana

 KIUKWELI hapa nimetoka kapa, yaani kwa hiyo Kimataifa uchumi umepaa lakini Kitaifa vyuma vimekaza? Mambo mengine ukifikiri sana unapata kizunguzungu. Ngoja nikanywe chai na panado kwanza

8 January 2018

CHEKA NA KITIME YABISHANA NA MAGAZETI 8 JANUARI 2018, wanawake wanaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kiume nao watandikwe mboko...........

 Oyaa ngoja kwanza ndugu mhariri, unaongelea mabasi haya haya au kitu kingine? Maana uvumbuzi huu lazima uwekwe kwenye kumbukumbu za kimataifa. Unajua ubunifu huu ni kundi moja na mtu aneweza kugeuza pasi ikawa friji, au redio ikawa tv. Ni muhimu mkuu ukaja na picha za hao wabunifu na pia kuonyesha pikipiki hizo wakaiti zikiwa bodaboda na baada ya kukarabatiwa na kuwa basi. Ulimwengu lazima ututambue safari hii, huko ndiko kutekeleza kivitendo kauli mbiu ya Tanzania nchi ya viwanda garemit usicheze na wabongo bwana, si sio wa nchi hii.

7 January 2018

CHEKA NA KITIME YABISHANA NA MAGAZETI 7 JANUARI 2018, baada ya mafuta ya ubuyu, mayai ya kwale, sasa ni mbegu za maboga

 Waziri Mkuu Uingereza eti kaja juu eti kwanini bodi ya parole imemuachia mbakaji aliyekaa jela miaka 9. Karibu Bongo Mheshimiwa Waziri ujifunze


 Oyaa Beckam usiwe unapenda kuchekesha watu sana unaona umevunja watu mbavu? Acha hizo mshkaji


 Aise mbona hili si jambo la ajabu sana, mbona ishu ya kupaa kwetu ni kitu cha kawaida, kijijini kwetu wazee wengi tu walikuwa wakipaa usiku kwenda kuloga, tena wao fasta, wanakwambia Ulaya hapa ni dakika chache tu. Inaonekana ungo aliyotumia mkuu ulikuwa sloo sana. Ila nimependa ishu ya kwenda kulala kwa Mbwana Samatta, analala kwa homeboy


 Kila siku nawaambia Kiswahili kigumu mnabisha hebu tafsiri kwa kiingereza sentensi hiyo hapo juu, andika hapo chini inbox, tukupime


 Mwongozo ndugu spika, naomba mwongozo......hii ishu imekaaje?


 Kweli bwana goma, si wakufungie na kadem flani kenye mvuto, sasa wanakufungia na TFF? Wala haina starehe


 Wangewateuwa chini kwa chini wangesikia jinsi ambavyo mimi ningelalalmika. Sipendi mambo ya chini kwa chini mimi.


 OK sasa nimeelewa ungo wa kusafiria unahitaji dreva, ni kweli kabisa ndio maana ili kupaa kwa usalama lazima na dreva awepo, ama sivyo dreva anaenda fanya nini Ubelgiji?


 Ayaaa jamaa wameshaharibu Jumapili yangu, waif aliniaga anataka kwenda kuwaona ndugu zake Kibaha, nimeshtuka hakuna kwenda Kibaha wala Mbezi, na sokoni naenda mwenyewe sitaki kuibiwa kindezindezi mimi.


 Ndio lazima akajibu mashataka ya mauaji, we unapoiua Yanga sasa Simba watacheza na nani? Simba hakikisheni huyo mtu anapata adhabu stahiki


 Sasa hatasijui niseme nini wakati mamluki wanaajiriwa kulinda nyumba ya ibada.....ngoja ninyamaze, jamaa hawachelewi kuanza kukemea kablog kangu kashindwe na kulegea


 Hahahahaha Wabongo kila mwezi wana kipa kiki kitu kipya, wameshapitia mafuta ya ubuyu, supu ya pweza, mayai ya kwale, Babu Samunge, sasa Mbegu za Maboga. Hahaha acha kula michipsi kutwa mwanaume, mbegu za maboga utakula weeeeeee wapiiiiii


 Hii ishu lazima nifuatilie maana nimeshaona dalili kabisa za kipara. Japo enzi zetu kipara cha uzee ilikuwa heshima siku hizi vibinti havitutaki wenye vipara


Mr Misifa wa Marekani jana kaita waandishi wa habari ajitetee kuwa yeye ana akili sana na akili yake iko ngangari. Wenzio wanakuteta mkuu wanasema wewe zumbukuku wametunga mpaka kitabu. Ene wei mi nasema walichosema usije ukakata misaada kwetu, nakumbuka nchi yenu ilitusevu sana na buluga

6 January 2018

CHEKA NA KITIME YABISHANA NA MAGAZETI 6 JANUARI 2018...mhariri akimbilia Kongo kutafuta studio

 KUTOKANA NA SABABU ZISIZOELEWEKA  MHARIRI WETU KATIMKA BAADA KUSOMA HIVI VICHWA VYA HABARI. KADAI ANAENDA KWA KABILA KUMUOMBA AMTAFUTIE STUDIO AREKODI SINGO YAKE.


 WAHENGA WA KULE NG'AMBO WALISEMA 'NYIE MWASUSA SIE TWALA'

 DAH APIA AISE, SASA AMEUMIA SANA?

 EBWANEEE JAMAA WAONGO HAWA, MAMAMAMAMAMAMAMA. YAANI HATA LA KUSEMA NIMEKOSA. HAWA JAMAA NI HATARI