HATUPIMI BANDO

WACHA TULALEEEEEE

WACHA TULALEEEEEE
WACHA TULALEEEEE

WADHAMINI

29 June 2016

JIUNGE NA CHAMA CHA KUPINGA WHATSAPP


MWAKA 2020  mjue kabisa kuwa nakuja kugombea Urais.  Tena niko tayari kufanya kazi hiyo bila mshahara, wala gari, ntakuwa napanda Bajaj, kwenda ofisini, na kwa taarifa ntaendelea kuishi ghetto langu hilihili, ili niwe karibu zaidi na wananchi wangu. Mimi sio mwanasiasa kwa hiyo maneno mengi sina nia na madhumuni ya kugombea urais ni kuhakikisha Whatsapp naipiga marufuku. Nataka niwataarifu mapema  hakuna kitu kinaniudhi kama whatsapp, yaani hii kitu ndilo jipu la kwanza nitakaloanza kulitumbua mara tuu baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kunitangaza Rais. Unajua hii kitu imefikia imewazuzua watu kiasi cha kwamba kuna watu wakiamka kitu cha kwanza ni kufungua whatsapp kucheki meseji, na wakishaanza siku basi ujue hapo kila dakika tano wanaangalia simu kama kuna mesej mpya. Mtu mmoja anakuwa kwenye magrupu kumi, na kila moja linatuma mesej hamsini kila saa na mtu anataka kuzisoma zote, yaani anafanya kazi saa ngapi? Hata kulala wengine hawalali vizuri kwa kutegeshea kusoma meseji, au kutuma meseji. Whatsapp ni jipu. Watu wanaogopa kuzima simu hata wakiingia kwenye ibada wanaogopa isije ikatokea mesej zikaingia wakati wamezima simu.  Kesho au keshokutwa naenda andikisha chama Chama cha Wapinga Whatsapp Tanzania-CHAWA.  Ndugu zangu jiungeni kwenye chama changu cha CHAWA tuliondoe jipu hili. We fikiria unamchangua mtu awawakilishe sehemu badala yake anatumia muda huo kuchati halafu anadai yuko kwa ajili yenu, utapeli mkubwa, wabunge wa chama changu hawatakuwa wanatumia whatsapp kamwe ili wahakikishe wanalinda maslahi ya wananchi. Unajua siku hizi unaweza ukawa umekaa na mpenzi wako kumbe anawasiliana na mpenzi mwingine na wewe uko hapohapo na picha utapigwa itatumwa  ikiwa na maelezo, niko na fala, unajua hilo?  Halafu kinachoniudhi kuliko yote ni hawa madreva wanaoendesha  huku wanachat, yaani hawa ndio ukisikia chizi fresh au kubwa jinga basi ndio hawa. Yaani jitu limesoma vizuri, lina pesa nzuri linaaminika kazini, lina gari zuri, lina familia inalitegemea halafu linachezea maisha yake na ya wengine kwa kuchati wakati linaendesha gari, yaani bila wasiwasi tulisaidie lisije likafa au likapata ulemavu na kutesa wanafamilia tupige marufuku chanzo nacho ni whatsapp. Wananchi wote tujiunge na CHAWA.

No comments: