NGOJA TUKUITIE MBUZI WA MZEE KITIME

Dreva kazimikiwa gari lake karibu na kijiji kimoja huko Sumbawanga. Akiwa kainama anajaribu kuangalia sababu ya tatizo hilo, ng'ombe mmoja akapita karibu;
NG'OMBE: Pole mzee, jaribu kuangalia plag kama zinachoma, ikiwa sio hivyo, cheki fyuzi....Jamaa akashtuka sana kusikia ng'ombe akiongea, basi akatoka mbio kuelekea kwenye kijiji, njiani akiwa anahema akakutana na jamaa wawili;
DREVA: Jamani nimekutana na ng'ombe anaongea
MWANAKIJIJI 1: Kwani ilikuwaje?
DREVA: Gari langu limezimika wakati najaribu kutengeneza akaja ng'ombe akaanza kuongea, ananiambia niangalie plag
MWANAKIJIJI 2: Ng'ombe mwenyewe rangi gani?
DREVA: Mweusi ana madoa meupe.... Wanakijiji wakaanguka kicheko kwa pamoja
MWANAKIJIJI 1: Hahahahahahaha kumbe ni yule, aise ng'ombe muongo yule kijiji kizima, toka lini akajua kutengeneza gari? Ngoja tukakuitie mbuzi wa Mzee Kitime yule ndio anaujuzi wa magari....JAMAA AKAZIMIA

No comments:

Powered by Blogger.