HE KUMBE UNA UGONJWA WA ZINAA?

Manesi wengine noma, jamaa alikuwa na appointment na dokta. Akamuendea nesi aliyekuwa akipokea wageni ambao walikuwa wengi wamejazana kwenye mabenchi wanasubiri huduma;
JAMAA: Samahani naomba kumuona dokta anishauri dawa vipimo hivi hapa...akampa nesi karatasi, nesi akasoma kile kikaratasi
NESI: ( Kwa sauti kubwa) He kumbe una ugonjwa wa zinaa, muwe na nyie mnajichunga jamani
JAMAA: (Nae kwa sauti) Sawa nesi, dokta alinambia na wewe ugonjwa huu ulikusumbua kwa muda mrefu sana, vipi dawa hizi zilikusaidia?

No comments:

Powered by Blogger.