DAKOKU NJOO UNIFUNGULIE

Dakoku alifunga Pub yake kama saa nane ya usiku kama kawaida, akafika kwake akiwa hoi, ile usingizi unaanza kumpata simu yake ikalia, sauti ya kilevi ikasikika;
SAUTI: Hallo mchumba, Pub yako unafungua saa ngapi?...... kwa hasira Koku akakata simu. Baada ya dakika chache ikalia tena
SAUTI: Hallo we dada, saa ngapi unafungua Pub yako husikii?. Mdada akakasirika;
KOKU: Sikiliza wewe acha kunisumbua na ujinga wako hata ningekuwa nimefungua nisingeruhusu mlevi kama wewe kuingia shenzi
SAUTI: Ngoja , mbona unapaniki, nani kakwambia nataka kuingia? Mi nataka kutoka umenifungia

No comments:

Powered by Blogger.