KILA KITU KIPO

Kijana alikuwa ana siku mbili toka aajiriwe kama mhudumu kwenye duka moja kubwa la vyakula akawa anaongea na mama mmoja mteja aliyemuuliza swali;
KIJANA: Mama kwa kweli hatuna kitu kama hicho katika duka hilo.....meneja wa duka kusikia hivyo akaingilia kati mazungumzo;
MENEJA: Mama, huyuu kijana bado mgeni ana siku mbili tu, hakuna kitu hatuna humu ndani.....mama akaondoka bila kusema hata neno
MENEJA: Sikiliza kijana kibiashara kamwe hausemi kama huna kitu, umenisikia nilivyojibu kitaalamu, jifunze kwangu. Haya yule mama alikuwa anataka nini?
KIJANA: Alikuwa anauliza kama humu ndani hatuna panya

No comments:

Powered by Blogger.