NAITWA FALA

Jamaa alikuwa safarini usiku gari lake likaharibikia kwenye kijiji kimoja, akagonga nyumba moja wakamfungulia, baada ya kueleza tatizo lake wakamkaribisha ndani, akapewa maji ya kuoga na chakula kizuri;
MZEE: Sasa huyu jamaa sijui alale wapi?
MKE: Saa hizi ni usiku akalale na Bebi...jamaa akaona huyo Bebi atamsumbua pengine atamkojolea usiku au atakesha analia.....
JAMAA: Msipate tabu mi ntalala hapahapa sebuleni.. akalala mpaka asubuhi. Wakati anakunywa chai akatokea binti mzuri sana, hata jamaa akawa anashindwa kuacha kumuangalia.
BINTI: Naitwa Bebi, we unaitwa nani?
JAMAA: Ahhhh mimi naitwa Fala

No comments:

Powered by Blogger.