Akina mama wawili waliosoma pamoja walikutana sokoni baada ya salamu;
ISABELA: Jamani Adela vipi mwanao?
ADELA: Kwa kweli mwanangu kaoa mwanamke mchawi, kamloga kamuinamisha
mwanangu, we fikiria, mwanamke anaamka saa 5, akiamka hapo ni kuzurula mji
mzima kutumia pesa za mwanangu, mwanangu akirudi kachoka jioni, hakuti chakula,
badala yake hao wanaenda kula kwenye mahoteli ya gharama, yaani we acha tu. Vipi
binti yako?
ISABELA: Mtoto wangu kaolewa na malaika, mwanaume anaamka alfajiri
anamtengenezea binti yangu chai anamletea chumbani, anamuachia pesa nyingi za
kutumia kwenda kununua anachotaka, kila siku akirudi anampeleka kula kwenye
hoteli za gharama maisha yao kwa kweli mazuri sana












0 COMMENTS/TUMA MAONI:
Post a Comment